Moja kati ya habari zilizoshitua wengi usiku wa February 23 2017 ni pamoja na habari za uongozi wa
Leicester City kutangaza kuamua kumfuta kazi rasmi aliyekuwa kocha wake mkuu wa
Claudio Ranieri,
Leicester City wamefikia maamuzi hayo kufuatia kutofanya vizuri katika Ligi Kuu
England.

Claudio Ranieri
Claudio Ranieri anafutwa kazi na
Leicester City ikiwa ni siku moja imepita toka apokee kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa
Sevilla katika mchezo wa UEFA Champions League,
Ranieri amefutwa kazi zikiwa zimepita siku 298 toka aipe Ubingwa wa
England Leicester City kwa mara ya kwanza katika historia.
Leicester msimu huu imekuwa ikiyumba kutoka kutwaa taji la EPL msimu wa 2015/2016 hadi kushika nafasi za kuwania kutoshuka daraja, kwa sasa ipo nafasi ya 17 katika Ligi Kuu
England na ilipoteza na timu ya
Millwall kutoka League One katika mchezo wa
FA Cup msimu huu.
Hadi sasa
Leicester City imecheza jumla ya mechi 25 katika Ligi Kuu
England, ikiwa imebakiza jumla ya mechi 13, imeshinda jumla ya mechi 5, sare mechi 6 na imekubali vipigo katika mechi zake 14 msimu huu na ina point 21 ikiwa katika hatari ya kuwania kutoshuka daraja.
No comments:
Post a Comment