News

  MFUNGWA AMBAKA MWANAFUNZI WA SHULE YA  MSINGI HUKO GEITA

 
MFUNGWA aliyekuwa akitumikia kifungo cha miezi sita katika Gereza la Butundwe wilayani Geita amembaka mwanafunzi wa Shule ya Msingi Luhuha iliyoko Tarafa ya Butundwe na kumuumiza sehemu zake za siri, shingoni na kwenye jicho la kulia.
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 15 (jina linahifadhiwa) alitendewa unyama huo na mfungwa aliyejulikana kwa jina la Godfrey Seleman (19) Februari 26, mwaka huu majira ya saa 9:00 alasiri wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akichanja kuni na wanafunzi wenzake.
Akieleza jinsi alivyofanyiwa unyama huo, mwanafunzi huyo alisema alipotoka shuleni akiwa na wasichana wenzake watano walikwenda kuchanja kuni ndipo walipomuona mfungwa huyo akiwa amevaa sare, lakini baadaye alitoweka ghafla na kurudi akiwa amejipaka masizi usoni, akiwa uchi kisha kuanza kumfukuza yeye huku wenzake wengine wakifanikiwa kukimbia huku wakipiga kelele.
Alisema alizidiwa mbio na mfungwa huyo ambapo alimshika kisha kumkaba shingoni na kumwangusha chini na kuanza kumtendea unyama na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri .“Baada ya kutendewa unyama huo nilitoka eneo hilo ambapo njiani nikutana na mama mmoja nikamwelezea mkasa ulionipata alinionea huruma ambapo alinipeleka ofisi ya kijiji ambako niliandikiwa barua kuwahi polisi, nikapelekwa hospitali ambako walinifanyia vipimo,” alisema binti huyo.
Aliendelea kusema kuwa mfungwa huyo alimpiga na kumuumiza katika jicho lake la kulia ambalo limevimba na kuwa bado anasikia maumivu makali jichoni na shingoni.Kamanda wa polisi mkoani hapa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo ameliita la kinyama lisilopaswa kutendwa na mtu mwenye akili timamu.Alisema mfungwa huyo mweye na namba 244/2013 alikuwa atoke kifungoni mwezi ujao, tayari ametiwa mbaroni na atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.

Odinga afikisha malalamiko mahakamani

Polisi mjini Nairobi, Kenya, wamefyatua moshi wa kutoza machozi kuwatawanya mamia ya wafuasi wa Waziri Mkuu Raila Odinga, nje ya mahakama makuu.

Mawakili wa Bwana Odinga waliwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mapema mwezi huu, ambapo Bwana Odinga alishindwa kwa kura elfu chache na Bwana Uhuru Kenyatta.
Hapo awali Bwana Odinga aliwasihi wafuasi wake wasijihusishe na vurugu.
Mawakili wa Bwana Odinga wamekwenda mahakamani wakidai kuwa kumepita udanganyifu kwenye uchaguzi.

Kanisa katoliki lapata Papa mpya

 

Kadinali Jorge Mario Bergoglio wa Argentina amechaguliwa kuwa Papa mpya wa Kanisa Katoliki.
Kadinali Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa Papa.
Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I.
Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa. Hii ilikuwa ni ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa kumchagua Papa mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao.
Kadinali Bergoglio anachukuwa mahali pa Papa Benedict XVI, ambaye alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.
Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne kwa siku.
Ilikuwa inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani theluthi-mbili wangeliweza kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa Papa mpya.
Na kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za kuonyesha nani angelichaguliwa.
Moshi mweupe
Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani walikwa wamekusanyika katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne.
Muda mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa .

Uhuru Kenyatta atangazwa rasmi kinara wa kiti cha urais wa Kenya


Tume huru ya uchaguzi na ukaguzi wa mipaka ya nchini Kenya IEBC imemtangaza rasmi Uhuru Kenyata kuwa mshindi wa kiti cha uraisi ikiwa ni baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu kura kutoka katika maeneo yote nchini humo.

No comments:

Post a Comment