WILAYA YA SENGEREMA YAPATA PIGO KUBWA KATIKA TASNIA YA MZIKI WA KIZAZI KIPYA BAADA YA KUONDOKEWA NA MSANII GODFREY MAKOYE.

                                                                   R . I. P
                                                            GODFREY MAKOYE.
                                           GODFREY MAKOYE ENZI ZA UHAI WAKE.
                              GODFREY MAKOYE WA PILI KULIA ALIEKAA NA LIDIA JUA KALI WAKIWA NA WASHIRIKI  WENZAKE WALIOINGIA KATIKA TANO BORA YA MASHINDANO YA KUIMBA WAKIJIANDAA NA FAINALI.

                     GODFREY MAKOYE WA KWANZA KUSHOTO AKIWA KACHUCHUMAA AKIWA NA SHILLAH ALIECHUCHUMAA na WA KWANZA KUSHOTO ALIE SIMAA NI BAD NAMBA, ANAEFATA NI IS HASLA NA RAMA BYSER WAKIWA WAMESIMAMA.
 GODFREY MAKOYE WA KWANZA KULIA ALIESIMAMA, AKIWA NA WASHIRIKI WENZAKE, WA KWANZA KUSHOTO ALIE CHUCHUMAA NI LIDIA JUAKALI, ANAEFATA NI BINGWA MAN  na WALIOSIMAMA WA KWANZA KUSHOTO NI SHABIKI WA BAD NAMBA NA ANAE FUATA NI KING SAMSON.


        Godfrey makoye enzi za uhai wake akiwa anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya MISSION kabla hajafikwa na umauti.                                                   

Tasnia ya mziki katika wilaya ya sengerema yapata pigo baada ya kuondokea na msanii wa kizazi kipya katika wilaya ya SENGEREMA ambae alivuma sana akitokea katika tamasha la kutafuta vipaji vya kuimba ambalo limekuwa likifanyika kila mwaka katika wilaya ya engerema ( SENGEREMA MUSIC and DANCE  TALENT SEARCH) ambalo lilianzishwa mwaka 2007 na GODFREY MAKOYE akiwa ni miongoni mwa wasanii wa kwanza katika mashindano hayo, hali iliyopelekea kuvuma sana kwa nyimbo zake mbalimbali ambazo zilitokea kupendwa sana na mashabiki wa mziki katika wilaya ya sengerema.                             

  GODFREY MAKOYE alifikwa na umauti akiwa anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya MISSION iliyopo sengerema baada ya kuwa anasumbuliwa sana na ugonjwa wa kuvimba miguu na kumfanya asumbuke kwa kipindi kirefu toka amalize ziara ya mikutano ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo alichukuliwa na mgombea wa CHAMA CHA MAPINDUZI mh. WILLIAM .M.NGELEJA, baada ya kampeni kuisha na uchaguzi kufanyika aliendelea kusumbuliwa na miguu hali iliyopelekea kupatwa na umauti uliomkuta tarehe 01/08/2016 katika hospitali ya mission.
          Kampuni ya EAGLE ENTERTAINMENT inatoa pole kwa ndugu ,jamaa na marafiki wa familia nzima ya marehemu GODFREY MAKOYE, na mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMINA.




                                           

No comments:

Post a Comment