NYUMBA YA MASHASHUA ILIYOPO KATIKA ENEO CHUO CHA FDC SENGEREMA YABOMOLEWA.

Nyumba ya mashashua yabomolewa baada ya danadana ya mda mrefu kati ya serikali na mumiliki wa nyumba hiyo mzee Mashashua.
  Kubomolewa kwa nyumba hiyo kumekuja baada ya kuonekana imejengwa juu ya bomba la maji ambalo linapeleka kaji katika tenki kubwa lililopo katika eneo la mlima wa chuo hicho cha FDC.
   Tenki hilo limekuwa likipokea maji kutoka katika ziwa victoria katika eneo la nyamazugo na kuyasambaza kwa wakazi wa mji wa sengerema, na kubomolewa kwake kumekuja baada ya wakandarasi kutaka kupitisha bomba katika eneo hilo ambalo ni la serikali kimsingi na kukutana na kizingiti cha nyumba hiyo ya mashashua ambae pia alikuwa na mtumishi wa serikali katika wilaya ya sengerema na ambae amewahi kukaimu nafasi ya mkurugenzi wa halmashauri ya sengerema ambae kwa sasa kaisha stafu utumishi wa umma.
   Eneo hilo limekuwa na mgogoro kwa kipindi kirefu hatimae leo tarehe 05/08/2016 limebomolewa rasmi.Na hapa nimekuwekea baadhi ya picha na nitaendelea kukuletea picha na kinachoendelea.



                                 Hapa ubomoaji wa nyumba ya mashashua ukiendelea.

No comments:

Post a Comment