Kwa mujibu wa kiongozi wa kikosi cha zima moto Bw.Juma Lundawa kutoka wilaya ya kinondoni ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ya moto imetokana na shoti ya umeme kwenye bweni la wasichana (Block B) katika chumba ambacho kinasadikika kuhifadhi magodoro ya wanafunzi.
Wanafunzi walioshuhudia moto huo wamesema moto ulianza majira ya saa mbili asubuhi huku jitihada za kuuzima moto huo zikiendelea mpaka kikosi cha zima moto kilipofika kuudhibiti moto huo.
Majeruhi wa tukio hilo ni wanafunzi wawili ambao wamepelekwa katika hospital ya kitaifa Muhimbili kupata huduma ya matibabu.
Hapa ni picha kutoka eneo hilo.
No comments:
Post a Comment