Kwa mujibu
wa kiongozi wa kikosi cha zima moto Bw.Juma Lundawa kutoka wilaya ya
kinondoni ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ya moto imetokana na shoti
ya umeme kwenye bweni la wasichana (Block B) katika chumba ambacho kinasadikika kuhifadhi magodoro ya wanafunzi.
Wanafunzi
walioshuhudia moto huo wamesema moto ulianza majira ya saa mbili asubuhi
huku jitihada za kuuzima moto huo zikiendelea mpaka kikosi cha zima
moto kilipofika kuudhibiti moto huo.
Majeruhi wa tukio hilo ni wanafunzi wawili ambao wamepelekwa katika hospital ya kitaifa Muhimbili kupata huduma ya matibabu.
Hapa ni picha kutoka eneo hilo.
No comments:
Post a Comment