Kama utakuwa unakumbuka mwaka jana rapper Quick Rocka baada ya kufungua studio yake mpya inayoitwa Switch Records alitangaza kuwa Nahreel ndiye atakuwa mtayarishaji (producer) wa studio hiyo mpya.
Kilichofuatia ni hiki ambacho kimekuwa kinasikika sana, eti ni kweli mastaa hao hawaelewani? Hizo zilizanza wakati ambao Nahreel aliondoka kwenye studio hiyo na kuamua kufungua ya kwake iitwayo The Industry.
Akizungumza na millardayo.com producer Nahreel alifunguka na kusema; “Kiukweli
is true sielewani na Quick Rocka na kwa sababu yeye anadai kuwa mimi
niliondoka studio kwake kiswahili bila kumtaarifu.. huenda ni kweli
niliondoka hivyo lakini Quick Rocka mimi hakuniajiri kama mwajiriwa
wake Switch Records.. sisi tulikuwa tunafanya kazi kiushikaji na mimi
nilikuwa na mipango yangu ya kufungua studio lakini pengine labda jamaa
hakupenda kile kitendo cha mimi kuondoka pale“– Nahreel.
“Natafuta
jinsi ya kukaa naye na kuongea kama binadamu ili tuyaweka haya mambo
sawa, nimekosa huo muda kukaa naye kutokana na shughuli za hapa na pale
lakini nitamtafuta mwenyewe Quick tuongee tuyamalize“– Nahreel.
No comments:
Post a Comment