MANENO YA NAHREEL KUHUSU ISHU YA KUTOPATANA NA RAPPER QUICK ROCKA, CHANZO NINI ? STORI ISIKILIZE HAPA



.
.

Kama utakuwa unakumbuka mwaka jana rapper Quick Rocka baada ya kufungua studio yake mpya inayoitwa Switch Records alitangaza kuwa Nahreel ndiye atakuwa mtayarishaji (producer)  wa studio hiyo mpya.
Kilichofuatia ni hiki ambacho kimekuwa kinasikika sana, eti ni kweli mastaa hao hawaelewani? Hizo zilizanza wakati ambao Nahreel aliondoka kwenye studio hiyo na kuamua kufungua ya kwake iitwayo The Industry.
Akizungumza na millardayo.com producer Nahreel alifunguka na kusema; “Kiukweli is true sielewani na Quick Rocka na kwa sababu yeye anadai kuwa mimi niliondoka studio kwake kiswahili bila kumtaarifu.. huenda ni kweli niliondoka hivyo lakini Quick Rocka mimi  hakuniajiri kama mwajiriwa wake Switch Records.. sisi tulikuwa tunafanya kazi kiushikaji na mimi nilikuwa na mipango yangu ya kufungua studio lakini pengine labda jamaa hakupenda kile kitendo cha mimi kuondoka pale“– Nahreel.
.
Hii ni picha ambayo Quick Rock alipost na kutangaza kuwa Nahreel ndiye official producer wa studio yake mpya Switch Records.
Natafuta jinsi ya kukaa naye na kuongea kama binadamu ili tuyaweka haya mambo sawa, nimekosa huo muda kukaa naye kutokana na shughuli za hapa na pale lakini nitamtafuta mwenyewe Quick tuongee tuyamalize“– Nahreel.

No comments:

Post a Comment