Waachieni waumini waamue- Kardinal Pengo
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema maaskofu hawana mamlaka ya kuwaamulia au kuwalazimisha waumini wao juu ya kuikubali au kuikataa Katiba inayopendekezwa.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Kardinali Pengo amesema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya Wanawake Wakatoliki Tanzania WAMATA, na kusema kufanya hivyo ni kuingilia uhuru wao hivyo ni vyema wakaachwa ili waamue wenyewe.
Kardinali Pengo amesema kuwa waraka uliotolewa na Jukwaa la Wakristo Tanzania PCT na Baraza la Mkanisa ya kipentekoste nchini kutoiunga mkono Katiba Inayopendekezwa ameusoma na ana uheshimu waraka huo lakini unaleta utengano katika taifa juu ya Wakristo kuchukua uamuzi dhidi ya Serikali.
Ameongeza kuwa waliotoa Waraka huo ni watu wakubwa waliokabidhiwa madaraka katika kanisa ambao hawapaswi kupuuzwa lakini matamko hayo yanaashiria mgawanyiko wa taifa kati ya wakristo na wasio kuwa wakristo.
Aidha Karnadali Pengo ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine amesema maaskofu kuwa na madaraka ndani ya kanisa hawana mamlaka ya kuwalazimisha waamini kutenda jambo, kinyume na lililoko ndani ya dhamira zao ni muhimu waachwe watende jishini Mungu anavyowaongoza kwenye dhamira.
Msimamo wa Kardinali ni kuwaachia waumini wakapige kura baada ya kuisoma kwa kina Katiba Inayopendekezwa na kutafakari kwa kina na kupata maongozi ya Mwenyezi Mungu na si kwaamulia wafanye nini wasifanywe kama watoto.

kwa nini pengo hakutoa maoni yake hayo katika vikao vya maaskofu kabla hawajatoa tamko, huo si usaliti?
ReplyDelete