NUH MZUWANDA KUMUOA SHILOLE

Staa wa Bongo Fleva,Nuhu Mzuwanda ameweka wazi mahusiano yake na msanii mwenzake,Zuwena Mohamed’Shilole’kwa wazazi wake na kwamba ana mpango wa kumuoa msanii huyo.Kwa mujibu wa baba mzazi wa msanii huyo aitwaye Mzee Mlawa amefunguka kwenye U heard na Soudy Brown amesema kuwa mwanaye huyo alimueleza kuwa anataka kumuoa mchumba wake huyo(Shilole).‘’Mi sina tatizo kama wamependana waache waoane tu nasubiri wajukuu tu’’alisema baba Nuh Mziwanda. Aidha amefunguka kuwa mkwe wake huyo alimuona Shilole kwenye picha tu na hajawahi kumuona live, na kuhusu suala la umri alisema kuwa kama wamependana hana tatizo,ila suala la kuchora tattoo alisema kuwa alifanya maamuzi ya haraka sana kuchora tattoo.

No comments:

Post a Comment