STAA wa Bongo Fleva,Rehema Chalamila’Ray C’ameendelea na harakati zake za kutoa elimu juu ya athari za madawa ya kulevya kwenye jamii. Hivi karibuni msanii huyo kupitia Ray C Faundatiaon alitembelea shule ya sekondari ya Makongo na kutoa elimu juu ya athari za madawa hayo kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Kupitia account yake ya Instagram aliandika hivi…Ray C Foundation ikitoa Elimu Juu ya athari za madawa ya kulevya katika shule ya secondary Makongo......na Ina mpango wa kuzunguka shule zote za secondary za Dar na mikoa yote ya Tanzania.Pamoja inawezekana Say No to drugs.... …. Ray C Foundation imetembelea shule ya Makongo Secondary na tumetoa uelimishaji wa madawa ya kulevya na athari zake,wanafunzi na walimu wamefurahi sana...Ray C Foundation Ina mkakati wa kuzunguka shule zote za secondary hapa Dar na ikiwezekana nchi nzima kwa ajili ya kutoa Elimu Juu ya athari za madawa ya kulevya....Pamoja Inawezekana….


No comments:
Post a Comment