STAA wa Bongo Fleva,Rehema Chalamila’Ray
C’ameendelea na harakati zake za kutoa elimu juu ya athari za madawa ya
kulevya kwenye jamii. Hivi karibuni msanii huyo kupitia Ray C
Faundatiaon alitembelea shule ya sekondari ya Makongo na kutoa elimu juu
ya athari za madawa hayo kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Kupitia account yake ya Instagram aliandika hivi…Ray C Foundation ikitoa
Elimu Juu ya athari za madawa ya kulevya katika shule ya secondary
Makongo......na Ina mpango wa kuzunguka shule zote za secondary za Dar
na mikoa yote ya Tanzania.Pamoja
inawezekana Say No to drugs.... …. Ray C Foundation imetembelea shule
ya Makongo Secondary na tumetoa uelimishaji wa madawa ya kulevya na
athari zake,wanafunzi na walimu wamefurahi sana...Ray C Foundation Ina
mkakati wa kuzunguka shule zote za secondary hapa Dar na ikiwezekana
nchi nzima kwa ajili ya kutoa Elimu Juu ya athari za madawa ya
kulevya....Pamoja Inawezekana….


No comments:
Post a Comment