Rwanda kuwahamisha wakimbizi wa Burundi
Serikali ya Rwanda imetangaza kwamba itawahamisha mara moja wakimbizi wa Burundi hadi mataifa mengine.
Waziri wa maswala ya kigeni Luoise Mushikwabo amesema kuwa ukosefu wa maelewano haukubaliki ,baada ya mjumbe mmoja wa Marekani kuzungumzia kuhusu ripoti kwamba Rwanda imekuwa ikiwapa mafunzo wakimbizi wa Burundi ili kukabiliana na serikali ya Burundi.Rwanda kwa sasa inawahifadhi makumi ya maelfu ya wakimbizi katika kambi.
Taarifa ya serikali imesema kuwa uwepo wao katika himaya yake,ikiwa ni karibu na taifa lao,ni hatari kwa wahusika wote.
Burundi kwa mara kadhaa imeilaumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi walio na lengo la kuipindua serikali ya Bujumbura.
Hatahivyo Kigali imekana madai hayo.
Hatahivyo imebainika katika eneo la maziwa makuu kwamba uwepo wao kwa kipindi cha mda mrefu karibu na taifa lao ni hatari kwa wahusika wote.
Taifa la Burundi limekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu Nkurunziza kutangaza mipango mwezi Aprili kuwania muhula wa tatu,ambao alishinda.Mamia ya raia wameuawa na wengine 230,000 kulitoroka taifa hilo.
Hakuna kambi nyengine zozote za wakimbizi zinazojulikana isipokuwa kambi ndogo za muda kwa wale wanaongojea kupelekwa katika kambi ya Mahama.
CHANZO BBC.




No comments:
Post a Comment