Moja ya ahadi kubwa alizoziweka Rais Magufuli tangu ameanza kazi na Serikali yake ya awamu ya tano iko ya kubana matumizi na kukabiliana na ubadhirifu.
Taarifa nyingine imenifikia kutoka Ikulu kuhusu maamuzi ya Rais Magufuli, kaamua kufanya maamuzi mengine kusimamisha watumishi watano, tuhuma zinaziwakabili ni matumizi mabaya ya pesa Serikali.
Waliosimamisha ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA, Dickson Maimu pamoja na wengine wanne ambao wanafanyiwa uchunguzi.
Wafanyakazi wanaofanyiwa uchunguzi ni hawa;
Joseph Makani– Mkurugenzi wa TEHAMA
Rahel Mapande– Afisa Ugavi Mkuu
Sabrina Nyoni– Mkurugenzi wa Sheria
George Ntalima– Afisa Usafirishaji
Taarifa zilizomfikia Rais zinaonesha kuwa NIDA
hadi sasa imetumia bilioni 179.6 ambazo ni kiasi kikubwa cha pesa huku
kukiwa na malalamiko ya wananchi kuhusiana na kasi ndogo ya utoaji wa
Vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na NIDA.
Kuna taarifa pia kuhusu Mabalozi ambao
muda wao umekwisha na wengine wameteuliwa kwenye nafasi nyingine, hivyo
wanatakiwa kurudi Tanzania… Mabalozi hao majina yao haya hapa.
Batilda Salha Buriani– Tokyo, Japan
Dk. James Alex Msekela– Rome, Italia
Peter Allan Kallaghe– London, Uingereza
Dk. Deodorous Kamala– Brussels, Ujerumani
Dk. James Alex Msekela- Rome Italia
Dk. Aziz Ponray– Kuala Lumpar, Malaysia
Francis Malambugi– Brasilia, Brazil
No comments:
Post a Comment