Mkali huyo alipofika TZA kwenye studio za Millard Ayo Sept 25 2015 alitaja sababu kwanini haonekani kwenye majukwaa ya kisiasa >>> ‘kusema kweli nimekuwa mzito sana kuona kama ni sawa au sio sawa yaani nimekuwa mtu ambaye niko slow sana, kuna wakati hata mtu akiniuliza Ben unafanya kampeni moyoni mwangu inanichukua muda mrefu kumjibu lakini sijapata majibu mpaka sasa mimi naangalia tu kama shabiki naona tu watu wanapost huyo mara huyo‘
‘Bado mpaka sasa sijajua nitampa nani kura ya Urais manake mwaka huu hivi vitu vinachanganya sana na sijui labda mpaka tusubiri tarehe 25 October nitapata ufumbuzi kamili kwenye kile chumba cha kupigia kura, ingekua kura zinapigwa leo ningekosa cha kuchagua, mimi kushiriki kuwafanyia kampeni Wanasiasa haitowezekana labda hela iwe kubwa sanaaaaaaa yani’ – Ben Pol
No comments:
Post a Comment