Zimenifikia taarifa za kuvamiwa kwa kituo cha Polisi stori iko hapa


mangu2
.
Ni taarifa ambazo zimechukua headlines usiku wa July 12 baada ya watu wanaosadikiwa kuvamia kituo cha polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga Dar na kuuwa watu saba.
Kwa mujibu wa Mkuu wa polisi (IGP), Ernest Mangu…’Nasikitika kuwapa taarifa kuwa majambazi walivamia kituo cha polisi cha stakishari na kupiga risasi na kuua Askari polisi wanne na raia watatu. Majambazi hao walikuja kama raia wakawaida  wanaohitaji huduma walipofika kituoni na kuulizwa shida yao nini ndipo walipoanza kuwashambulia askari walio kuwa kituoni’ – Ernest
.
.
‘Raia waliouwawa ni raia ambao walikuwa wamekuja kituoni kutoa taarifa za matukio ya kwao ya kawaida wapo pia askari ambao wamejeruhiwa na raia waliojeruhiwa wapo hospitali wanapata matibabu’ – Ernest Mangu
_MG_6074
‘Nikweli kuna silaha ambazo zimeporwa miongoni ni zile ambazo za askari ambao walikuwa ulinzi hapa na zingine zilikuwa chumba cha mashitaka.uchunguzi unaendelea kujua silaha ngapi zimeporwa wakati tukipata taarifa mpya tutazitoa’ – Ernest Mangu
.
.
‘Tukio hilo la kusikitisha lazima sheria ichukue mkondo wake kuwapata  hao waliohusika na tukio hilo.kama mnakumbuka tukio kama hili lilitokea Ushirombo walivamia kituo kama hiki walisababisha mauaji kwa Askari sisi hatutachoka tutahakikisha tunapambana nao mpaka tunawapata’ – Ernest Mangu

No comments:

Post a Comment