MANENO YA LINAH SANGA KUHUSU WATU WANAOMFATILIA MAISHA YAKE.

Mkorogo wangu unawahusu nini?- Linah Sanga
Msanii wa bongo fleva Linah Sanga amefunguka na kuweka wazi hisia zake za wazi juu ya watu ambao wanaomsema vibaya na kumkejeli kuwa huenda ameanza kujichubua.
"Jamanii nimechoka Na kufuru zenu, hivi naomba niulize ufupi wangu, kukomaa kwangu, mkorogo wangu vinawahusu nini? Ni naomba mfatilie kazi zangu tu vingine ni vitu vya kawaida kila binadamu kuumbiwa kasoro zake! Hivi wale ambao hawana mikono na miguu na wao walie vipi kwa Mungu? Namshukuru hivi nilivyo. Mbona mnapenda kutoa hukumu kama nyie ndiyo Israeli?! Ifike kipindi tukumbuke kila mtu anamaisha yake! Naona mnaniandamana sana na maisha yangu." amefunguka Linah
Una lipi la kumwambia Linah katika hilo?
East Africa Television (EATV)'s photo.

No comments:

Post a Comment