SHAMBULIO LA BALOZI WA MAREKANI KOREA KUSINI

AP_mark_lippert_hurt_02_jef_150304_16x9_992Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini Mark Lippert ameshambuliwa kwa kisu usoni na mkononi wake na mshambuliaji aliyekuwa akilalamikia kuhusiana na suala la kugawanywa ardhi ya Jumuiya yao wakati wa hotuba.
Balozi huyo alikimbizwa Hospitali ambako alifanyiwa upasuaji wa zaidi ya saa mbili kwenye jeraha na pia ameshonwa nyuzi themanini kwenye mkono uliokatwa, huku baadhi ya mishipa ikishindwa kufanya kazi ingawa madaktari wamesema hakuna athari yoyote itakayotokana na majeraha hayo.
Baada ya shambulio hilo maofisa wa Polisi walifanikiwa kumkamata Kim Ki-Jong akihusishwa na tukio hilo huku kukiwa na taarifa za jamaa huyo kufanya kosa kama hilo mwaka 2010 alipomshambulia Balozi wa Japan nchini Seoul.
Rais wa Marekani Barack Obama amempa pole Balozi huyo.
Msemaji wa baraza la maridhiano na ushirikiano ambaye ndiye muandaaji wa mkutano huo ameomba radhi kwa kutokuwa na ulinzi mzuri uliosababisha Balozi huyo kushambuliwa.
Mark Lippert
Mark-Lippert-AP-L
AP_mark_lippert_hurt_02_jef_150304_16x9_992 
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutu

No comments:

Post a Comment