Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya mabalozi wanaowakilisha wa nchi mbalimbali nchini Oman katika dhifa aliyoandaliwa na Naibu Waziri Mkuu wa Oman, Mhe. Sayyid Fahad Al Said (kulia) kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Naibu Waziri Mkuu wa Oman, Mhe. Sayyi Fahad Al Said (kushoto kwake) wakizungumza na balozi wa Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh katika dhifa aliyoandaliwa Waziri Mkuu kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 28, 2014. Wapili kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus kamani na watatu kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maalim Mahadhi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitembelea msikiti wa Sultan Qaboos Grand uliopo Muscut ambao ni kati ya misikiti mikubwa na inayovutia duniani Oktoba 29, 2014. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa serikali ya Oman, Ahmed Bin Salim Al Harthy.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka saini kitabu cha wageni baada ya kutembelea msikiti wa Sultan Qamboos Grand uliopo Muscut ambao ni kati ya misikiti mikubwa na inayovutia duniani Octoba 29, 2014. Kushoto ni Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa serikali ya Oman, Ahmed Bin Salim Al Harthy.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa serikali ya Oman, Ahmed Bin Salim Ali Harthy zawadi ya kitabu
kinachoonyesha Msikiti wa Sultan Qamboos Grand uliopo Muscut baada ya kuutembelea msikiti huo akiwa katika ziara ya kikazi nchini Oman.
kinachoonyesha Msikiti wa Sultan Qamboos Grand uliopo Muscut baada ya kuutembelea msikiti huo akiwa katika ziara ya kikazi nchini Oman.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akipokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Uhusiano wa Serikali ya Oman, Ahmed Bin Salim Al Harthy zawadi ya kitabu baada ya kutembelea msikiti wa Sultan Qamboos Grand wa Muscut ambao ni kati ya misikiti mikubwa na yenye kuvutia duniani.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Uhusiano wa Serikali ya Oman , Ahmed Bin Salim Al Harthy baada ya kutembelea Msikiti wa Sultan Qaboos Grand uliopo Muscut ambao ni moja kati ya misiki mikubwa na yenye kuvutia sana dunianiOktoba 29, 2014. Kulia ni balozi wa Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh.Yuko katika ziara ya kikazi nchini Oman.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa Oman kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut, Oktoba 29, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara wa Oman baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na mmoja wa wafanyabiara wa Oman wanaokusudia kuwekeza Tanzania, Sheikh Abdullah Al- Zakwani baada ya kikao chake na wafanyabiashara wa Oman kwenye hoteli ya Al Bustan, Muscut .
Moja ya barabara za jiji la Muscu, Oman.(Picha na Ofisi ya Waziri
No comments:
Post a Comment