WAKAZI WA HAPA SENGEREMA MJINI WAMEJIKUTA KATIKA HALI YA SINTOFAHAMU BAADA YA BARABARA ZA SENGEREMA MJINI KUJAZWA VIFUSI NA MKANDARASI KISHA KUVIACHA BILA KUVISAMBAZA KWA MDA WA WIKI MBILI SASA NA HAIJULIKANI NI LINI VITASAMBAZWA KWANI PAMOJA NA USUMBUFU UNAOJITOKEZA BADO WAHUSIKA HAKUNA HATUA YOYOTE INAYOONEKANA KUCHUKULIWA NA HAKUNA SABABU ZILIZOTOLEWA KIASI CHA KUWAFANYA WAKAZI WA HAPA MJINI KUBAKI NA MASWALI MENGI KICHWANI.
HII NDIO HALI HALISI ILIVYOKATIKA BARABARA INAYOKWENDA SENGEREMA SEKONDARI.
VIFUSI VIKIWA VIMEWEKWA KATIKATI KABISA YA BARABARA HALI INAYOPELEKEA BAADHI YA WANANCHI KUVISAMBAZA KAMA MUNAVYOONA.
BODABODA WAKIWA WAMEPAKI PIKIPIKI ZAO KATIKATI YA VIFUSI KAMA UNAVYOONA.
HAPA BAADHI YA WAMILIKI WA MADUKA WAKIWA WAMEVISAMBAZA BAADHI YA VIFUSI ILI KUWAWEZESHA WATEJA WAO KUPITA VIZURI LAKINI PIA BAADHI YA MAGARI YANAYOWAPELEKEA BIDHAA. TUNAPENDA KUTOA RAI KWA VIONGOZI WETU WA HALIMASHAURI YA WILAYA YA SENGEREMA MKURUGENZI NA MKUU WA WILAYA PAMOJA NA MADIWANI WETU WA HAPA MJINI KUHAKIKISHA VIFUSI HIVI VIKISAMBAZWA KWANI KWA WATU AMBAO WANAWEZA KUPATWA NA MATATIZO YA UGONJWA, WAJAWAZITO LAKINI PIA UNAPOTOKEA UHARIFU ITAKUWA SHIDA SANA KWA ASKARI NA MAGARI YAO KUFIKA KATIKA TUKIO KWA MDA.
No comments:
Post a Comment