Wakati Kamati kuu ya CHADEMA ikiwavua Uongozi Zitto Kabwe,Dr.Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba ,huu ndio Waraka uliowavua Vyeo.
Tundu Lissu.

Kamati kuu
ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema imewavua Uongozi Viongozi wake
watatu baada ya Kugundua waraka waSiri uliowahusisha na mpango wa
kukipasua Chama vipande vipande.
Viongozi waliovuliwa Uongozi ni Zitto Kabwe
ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Dr Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba
aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini.
Hatua hiyo ilichukuliwa katika kikao
cha kamati kuu kulichokuwa kimefanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Ubungo Plaza,
Dar es Salaam.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Mh Tundu Lissu amesema katika
Waraka huo kulikuwa na mtu anayejukana kama MM ambaye ni Naibu Katibu mkuu Zitto
Kabwe, M1 ni Dr Kitila Mkumbo, M3 ni Samsoni Mwigamba na M2 hajajulikana ambaye
ni mtumishi wa makao makuu ya Chadema.
Mh Lissu amesema Dr Kitila Mkumbo
alikana kabisa kumfahamu M2. Mh Tundu Lissu amesema Waraka huo uliojulikana
kama Waraka wa Ushindi unavunja katiba ya Chama kwa sababu umepandikiza chuki
za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na katiba ya CHADEMA.
Mh Tundu Lissu amesema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi
kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na
masharti ya katiba yetu. Mh Tundu Lissu Amesema Kamati Kuu imeamua kuwavua
nyadhifa zao zote watu wote waliotajwa katika waraka huo ambao ni Zitto Kabwe,
Dr. Kitila Mkumbo na SamsonMwigamba.
Pia kamati kuu imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia mhusika mwingine M2
ambaye anadaiwa ni Mtumishi wa Makao Makuu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa
dhidi yake.
Kamati Kuu imeagiza wahusika wote waandikiwe barua za kujieleza ni kwanini
wasivuliwe uanachama kwa makosa hayo makubwa waliyofanya.
Pia Kamati Kuu imeagiza mchakato wa kumvua Zitto nafasi yake ya Unaibu wa Kambi
ya Upinzani Bungeni.
Lissu amesema Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo waliomba
kujiuzulu nyadhifa zao zote baada ya waraka wao kukamatwa lakini Kamati Kuu
iliwakatilia baada ya kuona kuwa kukubaliana na maombi yao hayo ilikuwa ni kama
kuwaacha wajiuzulu kwa heshima ambayo hawaistahili hata kidogo.
Wakati huo huo kamati kuu imemteua Mh Tundu Lissu kuwa Mwanasheria mkuu wa
Chama.
MKAKATI
WA MABADILIKO 2013.
UTANGULIZI:
Zitto Kabwe.
Taasisi tunayoizungumzia ilisajiliwa rasmi mwezi January 1993 na tokea wakati
huo imeongozwa na wakuu wa taasisi wapatao wawili na aliyepo kwa sasa ni wa
tatu.
Wa kwanza aliongoza kwa miaka mitano tangu wakati huo 1993 hadi 1998 na
kumwachia aliyefuata ambaye naye aliongoza kwa miaka mitano hadi mwanzoni mwa
2004 na kumwachia aliyepo sasa. Huyu aliyepo aliongoza kwa miaka mitano tangu
mwaka 2004 hadi 2009 na kisha akachaguliwa tena mwaka 2009 kwa kipindi cha
pili.
Tunapenda
kwa hatua ya mwanzo kabisa kutambua juhudi za wakuu wetu wote waliopita
walizozifanya katika kuhakikisha taasisi yetu inakua kwa kutumia uwezo wote
waliokuwa nao na katika mazingira yaliyowakabili.
Mwaka 1995 chini ya mkuu wa
kwanza tulipata wawakilishi watatu kwenye chombo chetu kikuu cha uwakilishi.
Mwaka 2000 chini ya mkuu wa pili tukapata wawakilishi wanne pamoja na wa
nyongeza mmoja na kufanya idadi kuwa watano. Mwaka 2005 chini ya mkuu wa tatu
ambaye ndiye aliyepo hivi sasa, tulipata wawakilishi watano na wa nyongeza sita
jumla wakawa 11. 2010 chini ya mkuu huyu huyu wawakilishi wakaongezeka na kuwa
23 na wa nyongeza 25 na kufanya idadi kuwa 48 kabla ya kupata mwingine mwaka
jana na kufanya sasa wawe 49.
Tunapopongeza
juhudi zao hizi tunahitaji pia kuwapongeza wakuu wetu wawili wa kwanza ambao
kimsingi waliweka msingi mzuri sana wa kutong’ang’ania madaraka na badala yake
kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu.
Hawakuwa
madikteta na tunawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na
kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi
imara inayojali demokrasia na haki ya kila mwana taasisi.
Ni kwa msingi huo
waliamua kuandika kabisa katika mwongozo wetu kwamba kiongozi yeyote katika
ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi
kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea na kuongoza kwa kipindi cha
pili cha miaka mitano baada yapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile
aliyoitumikia kwa vipindi viwili.
Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema,
wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa
katika mwongozo bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.
Lakini kuna
matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza
kupata shida kubwa. Tunapenda kuainisha matatizo hayo kwa uchache kama ifuatavyo:
Wakati tukiufanyia mwongozo wetu mabadiliko mwaka 2006 hatukugusa kipengele
kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili
vya miaka mitano mitano. Lakini wakati mwongozo unachapwa chini ya uongozi
uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela.
Mambo yanayotokea hivi leo
yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na
kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa
kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu
katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo
mengine makubwa na yenye athari zisizomithirika kwa taasisi yetu.
Ni dhahiri kwamba uongozi uliopo umeishiwa mbinu na kuakisi jambo la msingi
sana ambalo waasisi wetu waliliona tangu mwanzo na kuamua kuweka kipengele cha
ukomo wa uongozi kwenye mwongozo wetu. Kuchoka kwa uongozi wetu kunaonekana
dhahiri katika mipango na mikakati ya taasisi ya miaka kadhaa.
Mfano mwaka 2008
uongozi ulianzisha mkakati wa operesheni samaki mkubwa (maarufu kama Oparesheni
Sangara). Huo ulifanyiwa kazi katika mikoa kadhaa na hatimaye ikafa kimya
kimya.
Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kulianzishwa matembezi ya
maandamano ambayo nayo yalikuwa yakipeleka ujumbe kwa watu na yalipangwa
kufanyika mikoa yote na wilaya zote.
Kumbukumbu zetu zinaonyesha kwamba yalikuwa yakianzia makao makuu ya mkoa na
kwenda kwenye wilaya zote. Lakini kumbukumbu hizo zinaonyesha kwamba
yalifanyika Mwanza, Musoma, Shinyanga, Kagera na mikoa ya Nyanda za Juu kusini
(Mbeya, Iringa, Njombe na Rukwa) kisha nayo yakafa kifo cha mende.
Dk. Kitila Mkumbo.
Kisha mwaka
2012 ikaanzishwa operation ya mabadiliko maarufu kama Movement for Change
(M4C).
Hiyo ilikuwa inakwenda kwenye mikoa na timu kama nne hivi ambazo kwa
ujumla zilitathmini hali ya mtandao na uongozi wa taasisi, kuhamasisha umma kwa
njia ya mikutano ya hadhara, kuingiza wanachama na kusimika uongozi na hatimaye
kufanya mafunzo kwa viongozi.
Hiyo ikafanyika Mtwara na Lindi, Morogoro na
kisha ikaenda kufia Iringa.
Mwaka huu viongozi wetu wamekuja na ugatuaji
madaraka kutoka makao makuu ya taasisi na kupeleka madaraka kwenye kanda
mbalimbali.
Mkakati huu ulikufa kabla ya kuanza pale viongozi wakuu
walipobadilisha maazimio ya kikao kikuu na kutekeleza matakwa yao ikiwa ni
pamoja na kuleta suala la viongozi wa muda kwa muda mrefu badala ya kuajiri
maofisa na wakahakikisha wanaweka watu wao kwenye uongozi wa muda.
Kitendo hiki
kwa peke yake, cha kufeli kwa kila mkakati unaoletwa na viongozi wetu katika
hatua za utekelezaji unaofanywa na wao wenyewe waleta mkakati, ni kiashiria
tosha kwamba uongozi uliopo umechoka.
Performance yetu kwenye chaguzi ndogo nayo ni ishara kwamba mabadiliko
yanahitajika. Tangu uongozi huu uingie madarakani, kumefanyika chaguzi ndogo 8
za wawakilishi kwenye chombo kikuu, kati ya hizo tumeshinda 2 tu sawa na
asilimia 25.
Aidha baada ya mwaka 2010 kumefanyika chaguzi kadhaa za
wawakilishi kwenye halmashauri.
Mwezi Oktoba 2011, mwezi wa4 2012, mwezi
Septemba 2012 na mwezi Juni 2013. Kote performance yetu imekuwa poor
kupindukia. Mfano mwezi wa Juni 2013 tumepata viti 6 kati ya 22 (27%) na mwezi
Septemba 2012 tulipata viti 7 kati ya 29 (24%).
Ni dhahiri mabadiliko
yanahitajika kwa kuwa wakuu waliopo wanatumia mbinu zile zile na kupata matokeo
yale yale. Tunahitaji mbinu mpya.
Kwa kifupi, ushindi ambao tumekuwa tukiupata
katika chaguzi ndogo haulingani na ukubwa wa hamasa kwa taasisi yetu iliyopo
mitaani. Hii ni kwa sababu tumekuwa tukitumia mbinu hizohizo katika kila
chaguzi.
Aidha, tu wepesi mno wa kuridhika na kujisifu kwa mafanikio madogo
badala ya kukaa chini na kutafakari kwa kina mahala tunapojikwaa.
Matumizi ya fedha za taasisi. Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama
zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani mkuu kabisa, mtendaji mkuu
na mkuu wa fedha kwenye taasisi yetu.
Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na
mabwana hawa.
Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina
ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya
uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti
yoyote yenye fedha.
Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine
ni maamuzi ya kikao cha juu mno cha hivi karibuni kilichoamua kwamba kiasi cha
fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa na wilaya na kiasi kingine
kipelekwe kwenye kanda.
Leo ni mwezi wa tano maamuzi hayo hayajatekelezwa.
Lakini kuna michango ya watu binafsi kama yule mtanzania mwenye asili ya
kihindi, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa
wapi na hatimaye zimetumikaje.
Hapo hatujataja fedha zinazopatikana kutoka
kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es salaam na Mwanza. Hizo
nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye
masuala ya fedha ni questionable.
Taarifa za fedha. Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao
chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na
matumizi ya fedha za taasisi.
Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua
mchezo huo ni watu watatu tu tuliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo
agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao.
Ni dhahiri
tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka
mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.
Kwa kiasi kikubwa mkuu
aliyepo anatengeneza mazingira yaleyale ya mwaka 2005 na 2010 ya kutaka chama
kiwe hakina hela ili ikifika wakati wa uchaguzi kimpigie magoti.
Kisha atatoa
pesa bila kumbukumbu zozote na mara baada ya uchaguzi anapeleka lundo la deni
na kudai alipwe hela aliyekikopesha chama wakati wa uchaguzi.
Alifanya hivyo
katika chaguzi za 2005 na 2010. Wakati wote wa kampeni za mwaka 2010, kwa
mfano, taasisi yetu ilihangaika sana kwa kukosa hata hela ya kununua maji kwa
wajumbe wa ngome.
Lakini ajabu ni kwamba baada ya uchaguzi mkuu wa taasisi na
baadhi wa wapambe wake walilete deni kubwa la takribani shililingi milioni mia
tano akiadi kuwa walikikopesha chama. Taasisi imewalipa pesa zote hizi kwa muda
mwaka mmoja. Sasa anatengeneza mazingira hayohayo kwa ajili ya uchaguzi wa
mwaka 2015.
Samson Mwigamba.
Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama. Wakuu waliopo
hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada.
Wanachokijua ni kukusanya
‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa
matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio.
Mawazo mazuri kama lile la kuanzisha kampuni la uwekezaji la taasisi yetu
litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, na hivyo
uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndoto ya
mchana. Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa
hapa jirani juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama
wamejifunza chochote.
Njia haramu za kubaki madarakani. Ili kuhakikisha wakuu wanabaki madarakani,
wameanzisha vikundi vikundi ndani ya taasisi yetu. Siku hizi ni rahisi sana
kuambiwa kwenye taasisi yetu eti huyu ni wa boss na huyu ni wa dogo.
Na wale
walio wa boss kwa kuwa boss ndo anashikilia raslimali za taasisi anatumia mfumo
haramu kuwaneemesha watu wake kwa kutumia raslimali za taasisi na kuwakandamiza
wote wanaoonekana wanapishana naye kimtazamo.
Jambo hili limewaibua wachumia
tumbo, wapenda madaraka, na vibaraka lukuki wanaokwenda kujipendekeza kwa wakuu
wa taasisi kwa malengo ya kujinufaisha binafsi. Katika kufanya hivyo vibaraka
hao wamekuwa wakiwaendea wakuu wa taasisi na kuwajaza maneno mabaya dhidi ya
viongozi wenzao na kuzidi kuwafarakanisha viongozi wa juu.
Kuna mchezo umeanzishwa na wakuu wa taasisi unaitwa ulinzi wa chama
uliogawanyika katika makundi mawili yaani visible na invisible.
Visible ni ule
unaoonekana ambao uko chini ya kikosi chetu chekundu ambacho kinajulikana kwa
kila mtu lakini invisible wanajulikana kwa mkuu wa taasisi na mtendaji mkuu
peke yake.
Wanafanya kazi kwa maelekezo ya wakubwa hao wawili na hawajulikani
kwa viongozi wengine wa juu. Ni hawa hawa ambao wanatumika vibaya pale
wanapoleta taarifa za kiintelijensia ambazo zinawahusisha viongozi wasiopendwa
na wakuu na usaliti dhidi ya taasisi.
Hakuna kamati maalum inayowathibitisha
maaintelijensia hao bali wakuu wenyewe wanawachukua wanaowataka.
Ni katika
mfumo huu wa kipuuzi mida eight amekuwa akitumika vibaya kwa kumshambulia
mtendaji mkuu msaidizi hadharani kwa kutumia mitandao ya kijamii na wakuu
wanafurahia na kumlipa pesa.
Udhaifu wa utendaji wa mtendaji mkuu. Mtendaji mkuu ni dhaifu mno na ni mara
nyingi sana tumeshuhudia mkuu wa taasisi akifanya mambo ya kiutendaji kinyume
na utaratibu kama vile yeye mwenyewe kuja kwenye kamati ya makatibu na
wakurugenzi na kupangua mipango yao na ku-inject ya kwake na mtendaji mkuu
kuadopt tu kana kwamba yeye hawezi kupanga mambo ya kiutendaji, hata tunapokuwa
kwenye operesheni maalum tumeshuhudia mkuu wa taasisi ndo akipanga watendaji,
posho zao na hata kusimamia matumizi ya pesa na shughuli mbalimbali za
kiutendaji.
Udhaifu wa mtendaji mkuu ni udhaifu wa mkuu wa taasisi kwa kuwa
amemteua yeye mara mbili tena mara ya pili alileta jina moja mbele ya Baraza la
juu kuonyesha kwamba aliridhika na utendaji wake kiasi cha kutotaka
kumpambanisha na mwingine.
Lakini baada ya kumpendekeza mara ya pili ndipo
tumeshuhudia yeye kuingilia kati mara nyingi sana mambo ya kiutendaji kana
kwamba anamfichia aibu mtendaji wake.
Swali kwa nini alimteua tena? Jibu lake
litakuwa rahisi tu kwamba ni kwa sababu mtendaji huyu ni passivekwa kila takwa
la mkuu wake.
Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi. Taasisi yetu
inayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya kamati ya makatibu na wakurugenzi.
Lakini uzoefu unaonyesha kwamba kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya
na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa
wakuu, wamekubali kuzimwa.
Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato
wa manunuzi ya magari, pikipiki, vifaa vya kueneza taasisi, set ya televisheni
iliyofungwa ofisini kwa mtendaji mkuu, hawana. Manunuzi haya yote yote
yanafanywa na wakuu hasa hasa mkuu wa taasisi bila utaratibu wowote jambo
ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi.
Bila aibu, mkuu wa
taasisi ndio amekuwa mnunuzi wa vifaa vyote vya chama nje ya nchi kwa bei
anayoijua mwenyewe na ambaye haihojiwi popote.
Huu ni mfano wa wazi wa mgongano
wa kimaslahi jambo ambalo ni hatari kwa kiongozi mkubwa wa taasisi kama yetu
inayojitambulisha katika kupinga vitendo vya ufisadi na uvunjifu wa maadili ya
uongozi kwa ujumla.
Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya kueneza taasisi.
Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa
tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya taasisi na
taasisi inanufaika vipi na mauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya taasisi
vinauzwa. Jambo hili linajulikana kwa wakuu tu.
Mifumo ya uteuzi wa maofisa wa makao makuu ya taasisi imevurugwa na siku hizi
wakuu wa taasisi hasa mtendaji mkuu anateua na kutimua ofisa anavyotaka na mara
nyingi bila hata kamati ya makatibu na wakurugenzi kujua.
Mambo haya
yanafanyika mbele ya macho na masikio ya mkuu wa taasisi jambo ambalo linazidi
kuthibitisha kwamba mkuu na mtendaji mkuu wanajuana na wanafanya kwa kulindana.
NANI TUMUUNGE MKONO KUCHUKUA NAFASI YA
MKUU.
Baada ya utangulizi huo unaoonyesha kinagaubaga kwamba tunahitaji mabadiliko,
hatua iliyofuata ilikuwa ni kuangalia nani anaweza kuleta mabadiliko
tunayohitaji.
Ni vema ikazingatiwa kwamba mtu ambaye tungemuunga mkono lazima
awe ni mtu mwenye uwezo mkubwa kuliko tunayetaka kumtoa. Awe ana qualities za
kiuongozi na zaidi sana awe na uwezo wa kupambana na mkuu aliyeko.
Tukileta mtu
asiyefahamika sana kwenye mifumo ya taasisi yetu hata kama angekuwa mzuri kiasi
gani hatachagulika na mkuu aliyeko atarudi kwa urahisi na kuendelea kuididimiza
taasisi.
Katika kuchunguza ndani ya taasisi tuliridhika kwamba mtendaji mkuu msaidizi
ana sifa zote tulizozitaja hapo juu ingawa kila mwanadamu ana udhaifu wake. Ni
dhahiri pia kwamba udhaifu wa mtendaji mkuu msaidizi unarekebika kuliko wa mkuu
aliyepo. Kwa ujumla mtendaji mkuu:
Ni kiongozi anayeweza kuongoza taasisi bila kujenga makundi akijali zaidi kazi
ya taasisi kuliko maslahi binafsi.
Ameonyesha kwa vitendo kwamba hana maslahi binafsi kwa kuwa tumeshuhudia
akifanya kazi nyingi za taasisi bila kudai malipo kwa njia ya posho ama
vinginevyo.
Anaheshimika na viongozi wa ndani na nje ya taasisi jambo ambalo ni la muhimu
sana kwa ustawi wa taasisi na kwa yeye kuwa mkuu wa taasisi tunatarajia wakubwa
wengi sana kutoka nje ya taasisi yetu kuiamini na hata kujiunga nasi katika
kuhakikisha tunafanikisha lengo la taasisi.
Ni msomi wa kiwango cha juu na mwenye uwezo mkubwa katika kuchanganua mambo ya
kiuchumi, kisiasa, kijamii, kimichezo, nk jambo ambalo ni muhimu sana kwa kuwa
ni hatari kuwa na kiongozi asiye na ujuzi wa kutosha kwenye masuala kama hayo.
Ndani ya taasisi anakubalika kwa makundi yote ya vijana, wazee na akina mama.
Uongozi wa sasa wa taasisi yetu umefanya tuonekana kwamba taasisi yetu ipo kwa
ajili ya kuvuruga amani ya nchi. Yote hii ni kwa sababu tumekuwa hatuna mbinu
mpya za mapambano zinabadilikabadilika zaidi ya maandamano ya kila mara. Kwa
kuzingatia utamaduni wa watanzania wa kupenda amani, kuna haja ya kufuta hii
taswira na njia rahisi ni kubadilisha uongozi wa taasisi haraka iwezekanavyo.
Uelewa wake wa mambo ya kiuchumi ni muhimu sana kwa taasisi kwa sasa.
Tunahitaji kuja na vyanzo vipya vya mapato ikiwa tunahitaji kufanikiwa. Mkuu
aliyepo si kwamba ameishiwa bali hana mbinu za maana za kuiimarisha taasisi
kimapato kwa ajili ya malengo yake ya mbele.
Exposure kubwa na kukubalika katika siasa za kimataifa. Tunahitaji kiongozi
ambaye anazifahamu siasa za kimataifa na anayeweza kuungwa mkono na viongozi
wengi wa kimataifa. Ni hatari kutegemea utaweza kufanikisha malengo kama ya
taasisi yetu bila mpango kabambe wa kuungwa mkono na jumuia ya kimataifa.
Mpaka
hivi sasa hakuna mpango wowote wala hata mchakato wa maana kuwa connected na
jumuia ya kimataifa. Kiongozi wetu mkuu wa sasa yupo ‘too local’ na hana
mawasiliano yeyote ya maana na viongozi wengine katika kanda na kimataifa.
Ndio
maana mkuu huyo na mtendaji wake mkuu wamekuwa hawaonekani katika matukio makubwa ya kimataifa.
Hata katika kutoa maoni katika mambo makubwa ya kitaifa
na kimataifa viongozi hawa hawapo. Kwa kifupi kwa sababu ya aina ya viongozi
tulio nao, nafasi ya taasisi yetu katika nyanja za kimataifa haipo!
Aina na staili ya uongozi wa sasa wa taasisi yetu ni kina kwamba nchi hii haipo
hadi taasisi yetu itakapochukua dola. Yaani tunafanya mambo kama kwamba
tutaanza upya kabisa tukichukua dola.
Ni kwa sababu tumegombana na kila mtu
katika utawala wan chi, vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama. Ukweli ni kwamba
tutavihitaji vyombo hivi kabla na baada ya kuingia madarakani na ni ndoto
kudhani kwamba tutakabidhiwa nchi kwa kugombana na kila mtu.
Ni kwa sababu ya
mtazamo kama huu ndio maana wakuu wetu wa sasa hawaonekani kabisa katika
shughuli za kitaifa kama vile sherehe za uhuru wan chi, n.k.
Uwezo wa kuwaunganisha wasomi wa kada mbalimbali, wafanyabiashara wakubwa,
watumishi wa umma na sekta binafsi, nk katika kupata muunganiko wa mawazo na
kutoka na sera murua zinazogusa kila sekta. Hili la kuwashirikisha litaenda
sambamba na kutoa elimu kwa wote waelewe na watuunge mkono.
Tunasema hivi kwa
kuwa watu wa kada mbalimbali hawajaelewa sera zetu juu ya mambo yanayowahusu
mfano wafanyabiashara wakubwa, wawekezaji, wakulima, watumishi, wanafunzi,nk na
hivyo hawajawa tayari kutuunga mkono.
Kile kinachofanywa wakati wa uchaguzi kwa
njia ya ilani ya uchaguzi na elimu kutolewa kwa njia ya kampeni majukwaani
hakitoshi. Tunahitaji watu wajue tumeunda think tank kwa ajili hiyo na baadaye
wajue nini kimetokana na think tank hiyo ili wajadili na kutoa maoni na
hatimaye tutoke na kitu kinachokubalikwa na wananchi wote. Na tuna imani hilo
tunayempendekeza ana uwezo nalo.
Kubwa zaidi ni kwamba alishaiangalia taasisi yetu na kuona mambo yanayohitaji
mabadiliko na kujiangalia yeye na kuridhika kwamba ataweza kuleta mabadiliko
tunayoyahitaji na ndipo mwaka 2009 aliamua kujitosa kuutafuta ukuu wa taasisi
yetu kabla ya kuombwa kumwachia aliyepo.
SWOT ANALYSIS:
Kwa kutumia uchambuzi huu hapa chini wa uimara, udhaifu, fursa na vitisho ama
vikwazo dhidi ya mtu tunayempendekeza, utaweza kutuonyesha kama
tunayempendekeza ataweza kushinda vita iliyo mbele yetu.
Kama SWOT inavyotaka,
tutaangalia sifa njema alizonazo tunayemtaka ambao ndio uimara wake,
tutaangalia pia udhaifu wake, tutaangalia fursa alizonazo na mwisho
tutazingatia vitisho ama vikwazo vilivyopo.
Ni muhimu tukaeleza kwamba katika
SWOT analysis tunajikita kwa mambo yanayohusika moja kwa moja na uwezekano wa
tunayemtaka, kuchaguliwa. Kwa hiyo kwa mfano utakuta kwamba katika sehemu hii
hatutazungumzia sifa njema alizonazo tunayemtaka kama kiongozi lakini sifa hizo
zikawa hazina ushawishi wa kuwafanya wajumbe wa kikao cha uchaguzi kumchagua.
Uimara wa tunayemtaka:
Ingawa si mmoja wa waasisi wa taasisi yetu, lakini ni mwana taasisi mkongwe
akiwa amejiunga na taasisi yetu miaka miwili tu tangu ianzishwe na mwaka mmoja
tangu isajiliwe rasmi na serikali.
Zaidi ya kuwa mwanataasisi mkongwe, hajawahi kujiunga na taasisi nyingine hapo
kabla. Alijiunga na taasisi hii kabla hata haijajulikana kwa watu na alibaki
kuwa mwana taasisi mwaminifu hata pale taasisi zingine zilipoonekana kuwa imara
na maarufu zaidi ya hii.
Kutokana na vipengele ‘a’ na ‘b’ hapo juu, hakuna mtu hata mmoja anayeweza
kusema mtu huyu alikuja kwenye taasisi yetu kwa ajili ya kutafuta maslahi kama
vile uwakilishi kwenye chombo chetu kikuu cha uwakilishi hapa nchini.
Ni mvumilivu sana. Katika jitahada za wakuu waliopo kuhakikisha wanaendelea
kukalia viti vyao, wamejitahidi sana kumpaka matope lakini amevumilia.
Mahali
ambapo wengine wangeshakata tamaa na kuhama taasisi, yeye alibaki kuvumilia
mpaka imefikia wana taasisi wa ngazi za chini waliokuwa wanadanganywa kwamba
mtu huyu ni msaliti, wameanza sasa kushtuka.
Ana historia nzuri ya utendaji uliotukuka ndani na nje ya chombo cha
uwakilishi.
Ana uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii, utamaduni,
michezo, nk. Uwezo wake unachagizwa si tu na elimu yake ya darasani bali pia
vipaji na akili ya kuzaliwa.
Ni mzalendo wa hali ya juu anayeipenda nchi yake kwa moyo wa dhati.
Amethibitisha hilo kwa namna anavyolitetea taifa letu katika medani za
kimataifa na jinsi anavyolipigania ndani dhidi ya mafisadi na wasiolitakia mema
taifa letu.
Ni mwakilishi pekee aliyekuwa tayari kukosa mishahara ya miezi
kadhaa kwa kuamua kusimamia ukweli kwamba kuna ufisadi ulifanyika mpaka
akasimamishwa uwakilishi wake kwa mikutano kadhaa ya chombo chetu cha
uwakilishi.
Katika kuzidi kuonyesha alivyo mzalendo tunaweza kusema hapa kwamba ni kiongozi
pekee kutoka upande huu ambaye ameonekana sana kwenye mambo ya kitaifa kwa
mfano kulipigania taifa letu katika mambo ya kimchezo, kutumia gharama zake
kwenda nje ya nchi na kujifunza mambo mbalimbali yanayoweza kulisaidia taifa
katika sekta nyeti kama mafuta, gesi na madini, nk bila kusahau kwamba amekuwa
ndiye mwakilishi pekee aliyeongoza katika kuibua kashfa nyingi na nzito za
ubadhirifu ndani ya serikali hata kufikia mawaziri kadhaa kufukuzwa kazi.
Mambo hayo tuliyoyataja kwenye vipengele ‘e’, ‘f’, ‘g’ na ‘h’ yamemfanya kuwa
kiongozi wa kwanza kuwa maarufu sana katika taasisi yetu aliyewapiku hata
viongozi wa serikali kwa umaarufu. Hii ya umaarufu ni sifa muhimu sana
linapokuja suala la uchaguzi.
Uwezo wake wa kujieleza kwa kujenga hoja pale anapopewa nafasi. Hata pale
anapokuwa amepakwa sana matope na wenzake, anapopewa nafasi ya kujieleza huweza
kuwashawishi watu wengi wanaomsikiliza. Hii itamsaidia sana siku ya kujieleza
mbele ya kikao cha uchaguzi ambapo ataweza kupangua hoja zote dhaifu za kumpaka
matope.
Ana uwezo wa kuchangamana na makundi yote ambapo vijana humwona kama mwenzao,
wanawake humwona kama mtetezi wao wakati wazee humwona kama kijana mwenye
busara anayeweza kuelekeza kama kiongozi.
Ana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za chini kutokana na ziara
nyingi alizozifanya na kukutana na viongozi wa ngazi za chini akiwa katika
kuijenga taasisi hii. Mahusiano haya mazuri yanachagizwa na jinsi anavyotumia
muda wa kuongea na viongozi wa ngazi za chini kuzungumza kwa lugha ya upole na
kuelekeza viongozi wenzake bila kuwaonyesha dharau.
Si mtu wa kujipenda nafsi na katika kupambana umaskini wa watu badala ya
umaskini wake, alifikia kuzikataa posho wanazolipwa wawakilishi wakati
wakitekeleza majukumu ambayo kwayo wanalipwa na kuiomba ofisi ya chombo hicho
kuzipeleka posho hizo kwa watu maskini.
Ana limu nzuri sana aliyoipata katika vyuo vinavyoeleweka kitaifa na kimataifa
Ni kijana na hii ni taswira njema kwa sababu taasisi yetu inaungwa mkono sana
na vijana
Udhaifu wa tunayemtaka:
Maneno yake mara nyingine hayazingatii anayazungumza katika mazingira gani na
hivyo kuwasha masikio ya wanataasisi jambo linalompunguzia kukubalika kwake
taratibu.
Kama ilivyo kwa maneno, kuna matendo pia ambayo mara nyingine huyafanya bila
kuzingatia mazingira na wasikilizaji wake na hivyo kupunguza imani ya wana
taasisi kwake.
Hali ya ndoa ya tunayemtaka kutoeleweka
msimamo wake
Kuna wakati tunayemtaka hu-respondkwa taharuki kubwa dhidi ya mashambulizi
yanayoelekezwa kwake jambo linalomfanya achukue maamuzi yasiyo sahihi kwa
wakati huo. Kwa kifupi kuna wakati tunayemtaka huonekana kufanya maamuzi
kwaemotion zaidi badala ya kutulia kwanza na kutafakari kwa kina ikiwa ni
pamoja na kutafuta ushauri kwa wenzake kabla ya kurespond.
Jambo lililoelezwa katika ‘d’ hapo juu humfanya tunayemtaka wakati mwingine
kuonekana ana jazba sana kwa sababu akishataharuki na kuchukua maamuzi akingali
kwenye taharuki huwa ni rahisi sana kuonekana anajibu mapigo kwa jazba sana.
Ustahimilivu: yaliyotajwa
katika ‘d’ na ‘e’ hapo juu yanaashiria tunayemtaka si mstahimilivu sana sifa
ambayo inahitajika sana kwa kiongozi.
Uwazi: Katika taasisi zetu hizi ni muhimu sana kuepuka kufanya
mambo yote wazi wazi hata kama ni mema ama ni haki ya mhusika ama si makosa
katika jamii tuliyomo. Kuna mambo ambayo ni haki ya mtu mfano mahusiano binafsi
ya kimapenzi, kuwa na marafiki wa damu kutoka upande mwingine wa utawala, nk.
Lakini mambo hayo ni muhimu wakati mwingine ama kwa kiwango fulani yakafanywa
kwa siri kuepuka mitazamo potofu kwa unaowaongoza.
Fursa alizonazo tunayemtaka:
Utamaduni wa taasisi yetu wa kubadilisha wakuu wa taasisi kila baada ya vipindi
vifupi ili kuleta maono mapya kwenye taasisi unampendelea tunayemtaka.
Udhaifu ulioonyeshwa na uongozi uliopo chini ya mpinzani wetu katika kutekeleza
program mbalimbali za taasisi nyingi zikiwa zimebuniwa na wao wenyewe, pia ni
fursa kwa tunayemtaka.
Udhaifu mkubwa ulioonyeshwa na uongozi uliopo kwenye ugawanyaji wa raslimali za
taasisi kama vile fedha za ruzuku, michango mbalimbali ya wahisani na hata
vifaa vya uenezi.
Kujitokeza kwa tunayemtaka kutaonekana kama fursa kwa wanataasisi kufanya
mabadiliko makubwa na kuua kabisa ile propaganda ya kwamba taasisi yetu ni ya
kabila fulani ama eneo fulani kwa kufanya reference kwa uongozi wa taasisi.
Hoja ya uongozi uliopo kushindwa kabisa kusoma taarifa za fedha tokea 2010
ikifahamika kwa wapiga kura inaweza kuwa machinjio kabisa ya uongozi uliopo na
kumpa fursa kubwa tunayemtaka.
Imani ambayo wana taasisi wengi wanayo kwake. Utafiti mdogo unaonyesha kwamba
bado jina la tunayemtaka linatamkika sana midomoni mwa wanataasisi pale
wanapotajwa viongozi wa juu wa taasisi yetu.
Hii inaonyesha bado wana taasisi
wanayo imani kubwa kwake na kwa hiyo atakapopata fursa ya kupangua matope
aliyopakwa atakuwa na nafasi kubwa ya kuchaguliwa.
Mpinzani wetu hana historia nzuri ya utendaji uliotukuka ndani na nje ya chombo
cha uwakilishi. Hakuonyesha utendaji wowote wa pekee alipokuwepo kwenye chombo
mwaka 2000 -2005 na hata alipopewa uongozi wa upande wetu ndani ya chombo tokea
2010 hadi leo 2013 hajafanya lolote la kutukuka ndani ya chombo hicho.
Mpinzani wetu hana uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii,
utamaduni, michezo, nk. Si tuelimu yake ya darasani ni ya magumashi bali pia
vipaji na akili ya kuzaliwa havijaonekana katika maisha yake.
Uzalendowampinzani wetu unatia shaka akiwa hajaonyesha lolote la maana katika
kulitetea taifa letu kimataifa.
Ingawa ameshapata nafasi lukuki ya kwenda nje
ya nchi lakini mara zote akifika huko ni kuiponda tu nchi yake. Ingawa anayo
majukwaa ya kufanya hivyo akiwa ameshakuwa mwakilishi mara mbili kwenye chombo
chetu lakini hatujawahi kumsikia akiibua kashfa mahsusi ya ufisadi na
kuisimamia zaidi ya yeye mwenyewe wakati fulani fulani kutuhumiwa kwa ufisadi
mfano pale alipokopa kwenye shirika la umma na kugoma kulipa mkopo.
Katika kuzidi kuonyesha uzalendo hafifu wa mpinzani wetu tunaweza kuangalia
jinsi ambavyo mpinzani haonekani kwenye mambo ya kitaifa. Hii ni fursa kwa
tunayemtaka.
Mpinzani wetu si maarufu akilinganishwa na tunayemtaka na hivyo kumpa fursa
zaidi tunayemtaka kumshindani mpinzani wetu kwenye uchaguzi.
Uwezo wa mpinzani wetu wa kujieleza kwa kujenga hoja pale anapopewa nafasi ni
mdogo sana.
Mpinzani wetu hajazoea ushindani na changamoto. Ni mtu aliyezaliwa kwenye
utajiri na anadhani pesa ni kila kitu. Ukimnyang’anya pesa ukamwambia ashindane
kwa hoja hawezi na ndo maana anajaribu sana kuhakikisha anaingia mwenyewe
ulingoni bila kupingwa.
Kutokana na tuliyoyasema hapo juu kwenye ‘m’ ni dhahiri kwambapale mpinzani
wetu anaporushiwa kombora la kashfa anakuwa mzito kujieleza hata kama anapewa
nafasi ya kufanya hivyo na hii ni fursa muhimu kwa tunayemtaka.
Mpinzani wetu ni mgumu sana katika kuchangamana na makundi yote ambapo vijana
humwona kama si mwenzao kiumri na kifedha, wanawake humwona kama malaya
anayependa kutumia miili yao kujistarehesha wakati wazee humwona kama mtu
anayedhalilisha hata nafasi aliyopewa kwa kufanya uhuni waziwazi hata kuvunja ndoa
si ya kwake tu bali hata za watu wengine.
Mpinzani wetu hana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za chini
kutokana na dharau nyingi anazozionyesha pale anapokukutana na viongozi wa
ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii.
Hutumia muda mwingi kuwaponda
viongozi wenzake hata kufikia kutamka mara nyingi kwamba kama kiongozi hawezi
kujigharamia nauli na malazi ya kutoka mahali fulani kwenda mahali fulani kwa
siku kadhaa hafai kuwa kiongozi bila kujali kwamba kuna viongozi wetu wana moyo
na taasisi hii na ndo wameifikisha hapa ilipo lakini hawana uwezo wa kifedha na
hivyo kauli kama hizo za mkuu huyu huona kama anawadharau kwa kuwa yeye ni
tajiri.

Hii imemfanya kutopendwa na viongozi wengi wa ngazi ya chini hivi sasa
na kutoa fursa ya pekee kwa tunayemtaka.
Mkuu aliyepo amekuwa na mkakati unaoitwa kuondoa watu wa zamani. Jambo hili
linawaudhi sana viongozi wa ngazi za chini ambao wanaona kama baada ya
kuifikisha taasisi mahali ilipo kwa sasa wanaonekana hawana maana tena. Wengi
wamefikia kuapa kwamba kama mwendo ni wa kuwaondoa watu wa zamani basi na yeye
ni wa zamani lazima aondoke.
Mpinzani wetu amejionyesha dhahiri kujipenda na kujijali nafsi bila kujali watu
wa hali ya chini. Matukio mawili yanamwacha uchi katika hili pale alipolitangazia
taifa kwamba wawakilishi wetu wote hawatachukua posho za vikao halafu yeye na
wengine wote wanazichukua hadi leo na kumwacha mtendaji msaidizi peke yake. Na
la pili linalofanana na hilo ni pale alipotangaza kutotumia gari la serikali
ambalo ni la kifahari kisha akalirudia kimya kimya.
Kuwepo muhtasari wa kikao cha wazee ambacho mwaka 2009 kilimshauri tunayemtaka
ajitoe na kumwachia mkuu aliyepo na kumtaka mkuu aliyepo kumwachia tunayemtaka
katika uchaguzi ujao na wote wakasaini makubaliano hayo, nayo ni fursa muhimu
sana kwa tunayemtaka.
Mkuu aliyepo anaamini kwamba ameshamsambaratisha tunayemtaka na hivyo kwa sasa
amebweteka na hiyo inatupatia sisi fursa kuendelea kuimarisha mtandao wetu.
Kwa kuwa ni mwislamu. Hii ni fursa katika kupata kuungwa mkono na wanachama
waislamu ambao wamekuwa na kigugumizi wakidhani waislamu hawatakiwi katika
uongozi wa taasisi yetu.
Elimu ndogo na duni aliyenayo mpinzani wetu ambaye ndiye mkuu wa taasisi yetu
kwa sasa.
Kwa sasa ni kiongozi pekee katika nchi yetu anayeongoza taasisi kubwa
asiye na elimu ya shahada huku taasisi yetu ikiwa inaongoza kwa kuwa na wasomi
waliobobea katika kila nyanja.
Hii ni kejeli hasa kwetu sisi ambao tumekuwa
tukiwasema wenzetu kwamba ‘akili ndogo’ inaongoza akili kubwa. Kimsingi
tumekuwa tukijisema kwa kukubali kuongozwa na mtu mwenye akili ndogo.
Mkuu wa sasa kutokuwa na msimamo thabiti katika mambo ya msingi. Rejea swala la
maandamano ya kumshinikiza Kawambwa ajiuzulu na kujitoa katika mchakato wa
katiba.
Vikwazo dhidi ya tunayemtaka:
Sisi wenyewe tunaoandaa mkakati huu hatuna uhakika kama tunayemtaka yuko tayari
na yuko serious na business hii, na kwa hiyo huenda tusifanye kwa nguvu zetu
zote ikiwa hatutapata nafasi mapema ya kukutana na mhusika na akatuhakikishia
kwamba yuko serious.
Utayari wa mhusika mkuu kutekeleza yale tunayokubaliana. Inapotokea baada ya
kukubaliana sisi na yeye akapata ushauri tofauti na ukauona uko more genuine,
basi tuwasiliane kwamba nimeshawishika kufanya hivi badala ya vile
tulivyokubaliana kwa sababu hizi ama zile. Hii haitatukatisha tamaa tofauti na
kama tutakuwa tunapanga hivi halafu yeye anafanya vile bila maelezo yoyote.
Kitendo cha mkuu aliyepo kung’ang’ania kuendelea nayo ni kikwazo kwa kuwa baada
ya kuwa madarakani kwa miaka yote hiyo lazima amejipatia watu wanaomhusudu ama
kumpenda ama kumkubali na kuwepo wengine wanaoogopa tu kwamba mkuu aliyepo
akitoka taasisi itakufa hata kama hawana sababu yoyote.
Tunatazamia mkuu aliyepo atafanya vitendo vingi zaidi vya haramu katika
kumdhibiti tunayemtaka pale tunapoelekea kwenye uchaguzi wenyewe.
Raslimali za taasisi kutumiwa na viongozi waliopo katika kumsaidia mkuu aliyepo
wakati wa kwetu anatumia raslimali zake za mfukoni.
Propaganda chafu zilizokwishapigwa dhidi ya tunayemtaka zimepunguza imani ya
wanataasisi kwa tunayemtaka kwa kiasi fulani.
Baadhi ya mambo ambayo amekwishayasema ama kuyatenda nayo yameshawapunguzia
imani kiasi fulani wanataasisi mbalimbali.
Kutoonekana sana kwenye operations za taasisi yetu pia kumewapa wasiwasi baadhi
ya wanataasisi.
Muhtasari wa SWOT analysis unaonyesha kwamba strength na opportunities za
tunayemtaka ni nyingi sana zikilinganishwa na weaknesses zake na threats dhidi
yake.

No comments:
Post a Comment