MITIHANI YA KIDATO CHA NNE KUSAHIHISHWA UPYA

Habari leo hii kutoka bungeni zinaweza kuwa ni sehem nzuri ama habari nzuri kwa wanafunzi wengu huku baadhi wakiona kama ni mizinguo..
sababu inayonifanya kusema hiki, ni pale nilipowafikiria wale waliopata division 1, hofu itakua imetanda baada ya kauli ya wabunge walioteuliwa kufatilia ishu ya kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne 2011 / 2012, ambapo inaonekana kabisa kurudiwa kusahihishwa upya kwa mitihani hiyo
Taarifa ya tume iliyoundwa na waziri mkuu kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watahiniwa wa kidato  cha nne  imesomwa  bungeni  leo  na  Mh.Lukuvi.
Mh.Lukuvi.  amesema sababu zilizosababisha  wanafunzi  wafeli   ni upungufu wa waalimu, mazingira magumu a kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa  na  utaratibu  mbovu  wa  baraza  la  mitihani  uliotumika  bila  kuwashirikisha  wadau  wa  elimu
Mh.LukuviI amesema kuwa NECTA haikufuata vigezo vya kuwafaulisha wanafunzi kwa kufuata STANDARDIZATIONS na CONTINOUS ASSESSMENTS.
Hivyo  basi, matokeo  hayo  yamefutwa  na yatasahihishwa upya

No comments:

Post a Comment