Habari leo hii
kutoka bungeni zinaweza kuwa ni sehem nzuri ama habari nzuri kwa
wanafunzi wengu huku baadhi wakiona kama ni mizinguo..
sababu
inayonifanya kusema hiki, ni pale nilipowafikiria wale waliopata
division 1, hofu itakua imetanda baada ya kauli ya wabunge walioteuliwa
kufatilia ishu ya kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne 2011 / 2012,
ambapo inaonekana kabisa kurudiwa kusahihishwa upya kwa mitihani hiyo
Taarifa ya tume iliyoundwa na waziri mkuu kuchunguza sababu za kufeli
vibaya kwa watahiniwa wa kidato cha nne imesomwa bungeni leo na
Mh.Lukuvi.
Mh.Lukuvi. amesema sababu zilizosababisha wanafunzi wafeli ni
upungufu wa waalimu, mazingira magumu a kufundishia, idadi kubwa ya
shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa na
utaratibu mbovu wa baraza la mitihani uliotumika bila
kuwashirikisha wadau wa elimu
Mh.LukuviI amesema kuwa NECTA haikufuata vigezo vya kuwafaulisha
wanafunzi kwa kufuata STANDARDIZATIONS na CONTINOUS ASSESSMENTS.
Hivyo basi, matokeo hayo yamefutwa na yatasahihishwa upya
No comments:
Post a Comment