Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, hatimaye mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ameamua kujibu shutuma za Lady Jaydee dhidi yake. Ruge amekitumia kipindi cha Power Break Fast cha Clouds FM, kujibu rasmi shutuma hizo.
Amesema anasikitishwa na jinsi Jaydee anavyoendesha harakati zake na kudai kuwa anapigana kwenye vita isiyo sahihi.Ruge amewaasa wasanii wa Tanzania akiwemo Lady Jaydee kuzitumia vizuri fursa za kiuchumi zinazojitokeza na sio kupenda kulalamika.
“Turudi kwenye mstari wa kuziona opportunities, turudi kwenye mstari wa kusema kwamba leo tunataka kumzungumzia Jaydee akiwa na perfume, akiwa na lipstick kama jana iliyozinduliwa na Rihanna ambayo nikaambiwa kwamba stock ya lipstick mpya ya Rihanna iliyozinduliwa ilikwisha baada ya masaa matatu.
That’s how bigger brand is supposed to be, and that’s how powerful a brand is supposed to be katika namna ya kuunganisha na fursa zilizopo. Unapokuwa na jina tumia fursa, tumia opportunities zinazokuijia wewe kujiendeleza na kujikuza.
Lakini suala la kulaumiana halitatukuza kwasababu sisi ni radio binafsi, tutafanya kile tunachokifanya sisi kwa matakwa ya wasikilizaji wetu wengi zaidi, tukiiangalia faida kama motivation, tukiiangalia social responsibility kama motivation yetu ya pili, in the long run kuangalia tunakotaka kwenda kufikia strategy ambayo kampuni yetu inajiwekea.”
No comments:
Post a Comment