Baada
ya kukaa kimya kwa muda mrefu, hatimaye mmoja wa wakurugenzi wa Clouds
Media Group, Ruge Mutahaba ameamua kujibu shutuma za Lady Jaydee dhidi
yake. Ruge amekitumia kipindi cha Power Break Fast cha Clouds FM,
kujibu rasmi shutuma hizo.
Amesema anasikitishwa na jinsi Jaydee anavyoendesha harakati zake na kudai kuwa anapigana kwenye vita isiyo sahihi.Ruge amewaasa wasanii wa
Tanzania akiwemo Lady Jaydee kuzitumia vizuri fursa za kiuchumi
zinazojitokeza na sio kupenda kulalamika.
“Turudi
kwenye mstari wa kuziona opportunities, turudi kwenye mstari wa kusema
kwamba leo tunataka kumzungumzia Jaydee akiwa na perfume, akiwa na
lipstick kama jana iliyozinduliwa na Rihanna ambayo nikaambiwa kwamba
stock ya lipstick mpya ya Rihanna iliyozinduliwa ilikwisha baada ya
masaa matatu.
That’s
how bigger brand is supposed to be, and that’s how powerful a brand is
supposed to be katika namna ya kuunganisha na fursa zilizopo.
Unapokuwa na jina tumia fursa, tumia opportunities zinazokuijia wewe
kujiendeleza na kujikuza.
Lakini suala la kulaumiana halitatukuza
kwasababu sisi ni radio binafsi, tutafanya kile tunachokifanya sisi kwa
matakwa ya wasikilizaji wetu wengi zaidi, tukiiangalia faida kama
motivation, tukiiangalia social responsibility kama motivation yetu ya
pili, in the long run kuangalia tunakotaka kwenda kufikia strategy
ambayo kampuni yetu inajiwekea.”
No comments:
Post a Comment