SPIKA AMEAHIDI KUWASHITAKI POLISI WABUNGE WANAOTUMIA MATUSI BUNGENI
Spika wa Bunge bi Anne Makinda amewashambulia wabunge leo asubuhi na kuwaambia suti zao walizovaa haziendani na matusi yanatoka katika vinywa vyao ambayo yeye ameshindwa kuyataja kutokana kwa madai kuwa mdomo wake hauwezi kutamka matusi hayo..... Makinda amesema matusi ndiyo yamekuwa yakitawala katika midomo ya wawakilishi hao na kuacha hoja inayojadiliwa hewani.... Spika wa bunge amekwenda mbali zaidi na kuwaambia wabunge hao kwamba hataangalia chama endapo mbunge atavunja kanuni za bunge kwa kuwa kanuni za bunge zinampa nafasi ya kuita polisi na kuja kumchukua.
No comments:
Post a Comment