Pages - Menu
The Magazine
MGANGA WA KIENYEJI AKAMATWA KATIKA SHULE YA MTAKATIFU KAROLI SENGEREMA (ST CAROLI SCHOOL).
Mganga wa kienyeji amekamatwa tarehe 17/05/2016 katika shule ya st. caroli school sengerema baada ya kuonekana akiwashawishi wanafunzi kutoa pesa ili kuwaongezea akili na uelewa darasani.
Tukio hili imetokea siku ya jumanne katika shule hiyo baada ya kuwashawishi wanafunzi kutoa kiasi cha tsh.20000/: kwajili ya kuwapatia dawa na hasa katika kipindi hiki ambacho tayari wapo katika mitihani ya kufunga, baada ya kukubaliana baadhi ya wanafunzi walitoa kiasi kidogo cha pesa kwajili ya kununulia dawa hivyo basi baada ya kwenda na kununua dawa alirudi sikuya jumanne kwajili ya kuanza kuwapatia dawa kitu ambacho tayari uongozi wa shule ulikuwa umeshapata tarifa ya utapeli huo hali iliyowafanya wandae mtego wa kumkamata haliiliyosaidia kukamatwa kwa mganga huyo na kupelekwa katika vyombo vya dola ili afikishe mahakama kwa taratibu zingine za kisheria kuchukua mkondo wake.
Rai yetu kwa waganga wa kienyeji kujiepusha na vitendo kama hivyo kwani vitamfanya mwanafunzi asijisomee na kutegemea waganga wa kienyeji na dawa zao hali ambayo inaweza kuleta mgogoro kati ya wanafunzi na walimu na wazazi na uongozi wa shule kwani inaweza kupelekea kiwango cha elimu kwa mwanafunzi kupungua siku hadi siku hali ambayo itamfanya mzazi kuhisi shule na walimu hawafundishi watoto wao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment