Makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya visiwa vya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameishutumu serikali ya Tanzania kwa kufumbia macho makundi yanayowavamia na kuwapiga wafuasi wa chama cha upinzani cha CUF
Mkuu wa polisi kisiwani Zanzibar, Kamishna Hamdan Omar Makame amezikanusha tuhuma hizo na kuhoji kuwa iwapo kuna watu walioshambuliwa ni kwa nini hawajashtaki.Chama cha CUF kimeendelea kusisitiza kuwa kilishinda katika uchaguzi uliopita na hivyo hakitashiriki katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 20 Machi na serikali iache kufanya hujuma zitakazoivuruga nchi.

No comments:
Post a Comment