“Video yangu ya Akadumba ni moja kati ya video zangu bora sana, muziki wangu unapendwa sana uswahilini kama kwetu Manzese. Hivyo basi kurekodi video kwenye mazingira yetu yale ya mtaani inaongeza mapenzi kwa mashabiki wangu. Labda nifanye kama nilivyofanya na Akadumba kumleta director mkali aje ku-shoot kitaani. Lakini sifikirii kwenda South Africa ku-shoot kwenye mazigira yao ya kishua wakati mashabiki wanafurahi kuona mitaa yao inarushwa kwenye video zangu. Kama niki-shoot video nje ya mazingira ya uswazi basi itakua ngoma tofauti sana lakini sio ngoma kama hii mpya Nyumbani Kwetu”.
Kwenye hatua za kutimiza haya maneno Nay wa mitego ametoa video ya Nyumbani Kwetu ambayo kwa kiasi kikubwa inaonyesha maisha na mazingira ya uswahilini. Enjoy kuicheki video yenyewe hapo chini.
No comments:
Post a Comment