CHADEMA WAPATA PIGO BAADA YA KUONDOKEWA NA MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA GEITA, MAWAZO ALPHONCE CHEMU.

 CHADEMA wapata pigo kubwa baada ya kuondokewa na mwenyekiti wake wa mkoa wa GEITA,bwana ALPHONCE MAWAZO CHEMU kilichotokea jana katika jimbo la busanda, kada huyo alifikwa na umati baada ya kuvamiwa na kundi la watu wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa silaha za jadi,tukio hilo lilitokea baada ya bwana mawazo akitoka katika kikao cha ndani cha viongozi ambacho kilikuwa kikifatilia shughuli za kampeni za kiti cha udiwani, katika kikao hicho kwa mujibu wa viongozi wa chadema mkoa wa geita walipata tarifa kuwa kuna watu wanakuja kuvamia kikao hicho hali iliyowafanya baadhi ya viongozi kuondoka akiwemo mawazo inavyosemekana alipanda bodaboda lakini kabla hajafika anakokwenda alivamiwa na kundi hilo la watu waliokuwa katika land cruiser.

TUNAPENDA KUTOA RAI KWA WATANZANIA HASA WATU WA JIMBO LA BUSANDA KUWA WATULIVU NA KULIACHA JESHI LA POLISI LIKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE,IKIWEMO KUWABAINI NA KUWAKAMATA NA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

No comments:

Post a Comment