Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC Paul
Makonda hii sio mara ya kwanza kuingia kwenye Headlines akizungumzia
tatizo la ajira, ndiye aliyeianzisha Kinondoni Talent Search ambayo
iliwakutanisha vijana wenye vipaji ili waoneshe uwezo wao na baadae
vipaji hivyo wavitumie ili iwe njia ya kujiajiri.
Zaidi ya vijana 1200 wamejitokeza leo kwenye viwanja vya Leaders ambapo DC Paul Makonda alitangaza kwamba anahitaji kukutana nao na kuangalia jinsi ambavyo wanaweza kuunganishwa na ajira kutokana na fani walizosomea.
Moja ya vitu ambavyo Paul Makonda
amevisisitiza ni kwamba vijana wanatakiwa kujitambua na hakuna ulazima
kila mtu awe ameajiriwa ila kunaweza kufanyika mbinu nyingine za
kujiajiri na kufanya biashara au ubunifu mwingine utakaowapatia.
No comments:
Post a Comment