Wengi tunafahamu kuwa muimbaji wa longtime kwenye muziki wa dance, Banza Stone anaumwa sasa leo millardayo.com ilimtafuta Mkurungezi wa kampuni ya ASET, ambaye ni mmiliki wa bendi ya African Stars aka Twanga Pepeta Asha Baraka kuzungumza machache kuhusu Banza Stone.
Akizungumza na millardayo.com alisema..‘Kikubwa
zaidi ni kuhusu Banza Stone, mimi mwenyewe niliwahi kumpeleka banza
mara mbili Hospitali, mara ya kwanza ilikuwa ni Muhimbili baadae
nikampeleka Mwananyamala huko ndio kuna msaada wa Ma Daktari lakini this
time imekuwa tofauti ambapo familia yake ina muuguza Nyumbani, kuuguzwa
nyumbani kwamba anapelekwa hospitali hizi za kawaida kisha anapewa dawa
anamezea nyumbani inakuwa pia ni tatizo kwa hiyo watu watahisi kuwa
sisi wasanii tunamtenga au hatukwendi nyumbani kumjulia hali yake
Hata
Juzi nilijaribu kuwashawishi wenzangu marafiki ambao ni wa karibu
wakaongee na mama Banza ili Banza Stone aweze kwenda hospitali kwasababu
mimi mwenyewe niliende ila sikuweza kufanikiwa kumpeleka hospitali
halafu nashindwa kumchukua mgonjwa akiwa ndani ya familia kumpeleka
hospitali kwani lolote linaweza likatokea kwa hiyo watu wasione kama
sisi tunamtenga Banza kuna ugumu pale namna kumtoa Banza kumpeleka
hospitali lakini tunaomba kama kuna mtu yoyote ana nguvu basi atusaidie
kumchukua Banza ampeleka hospitali..’alisema
No comments:
Post a Comment