WEMA NA PENNY WAMETANGAZA VITA NA DIAMOND NA MPENZI WAKE MPYA ZARI.
Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Wema
Sepetu na Mtangazaji Penniel Mwingila ‘Penny’ ambao wote kwa nyakati
tofauti wamewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond’ baada ya kuona habari za mwenza wao huyo wa
zamani akiwa na mpenziwe mpya, Zarinah Hassan zinapamba moto kila siku,
wameibuka na kudai hawababaishwi nazo, kwani hivi sasa wameamua kuingia
kazini kwa kufanya bonge la project
Akizungumza kwa niaba ya
mwenzake, Penny alisema kelele za kila siku wamezichoka na baada ya
kukaa pamoja, wameona hiki ni kipindi cha kupiga kazi badala ya kupoteza
muda.
“Tumeamua kuandaa filamu yetu ya pamoja ambayo ninaamini
itakuwa ni kali na ya aina yake. Tumepoteza muda mwingi na hivi sasa
tunahitaji kufanya kazi, tunachowaomba mashabiki wakae tayari kutupokea
na hatutaki tena kushabikia mambo ya Zari na Diamond kwa sababu
hayatuhusu,”
No comments:
Post a Comment