Dada mmoja aliyefahamika kwa jina la Jamila mkazi wa Kawe jijini Dar hivi karibuni alipata kipigo cha kufa mtu akituhumiwa kuchepuka na mume wa mwanamke mmoja aitwaye Sheila.Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo ilielezwa kuwa, Sheila alitonywa na wambeya kuwa Jamila amekuwa akichepuka na mumewe na bila kuchunguza akapanga kumshikisha adabu
“Jamila alikuwa akituhumiwa kutembea na
mume wa Sheila na siku ya tukio alifuatwa baa na kupigwa hadi kutaka
kutobolewa jicho,” kilidai chanzo.
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kuwatafuta wahusika ambapo Jamila alipopatikana alisema:
“Jamani ukweli ni kwamba mimi niliwahi kutembea na yule mume wa Sheila lakini tulishaachana sasa nimemshangaa mkewe kuja na kunipa kipigo sababu tu ya maneno ya kusikia”, alisema Jamila na kuongeza:

“Nilikwenda kufungua kesi Kituo cha
Polisi Kawe lakini siku chache baadaye Sheila alikuja na kuniomba
msamaha akidai kuwa alikosea kuamini maneno ya watu bila kufanya
uchunguzi. Tumesameheana na yameisha.
No comments:
Post a Comment