HUSSEIN MACHOZI AFUNGUKA BAADA YA KUZUSHIWA KIFO.


Baada ya kuzushiwa kifo na picha zake kusambazwa katika mitandao ya jamii Msanii Hussein Machozi amefunguka katika ukurasa wake wa Instagram na kusema haya
"watu wangu mimi ni mzima wa afya kabisa..sijakufa jamani..ni uvumi wa mitandaoni tu baada ya kufananishwa na mtu aliekufa kwa ajali huko Dodoma..Mimi niko salama salmini...ila hiki kitendo kimesababisha Mama yangu mzazi na dada yangu kuzimia kwa pamoja na hadi sasa wako hospitali kwa matibabu zaidi..kitendo hiki kimeniathiri hadi akili yangu jamani ..sio poa kuzua kitu kama hiki..ni mbaya sana....narudia tena sio mimi katika ajali ilio tokea Dodoma sio Mimi jamani...Nawapenda sana."
Kufuatia kuzushiwa kifo una neno lipi kwa Hussein Machozi?

No comments:

Post a Comment