Barnaba amefunguka kuwa hadhi yake haiwezi kushuka ndio maana kila siku anaendelea kuwa juu kwa sababu ana moyo wa kutoa kama Dini inavyosema ulichozidishiwa uwape wengine, anapenda kutoa support na furaha yake ni kuona mtu anasonga mbele kwa kupitia msaada wake, ameshaandika nyimbo nyingi kama za Lina, Recho, Mwasiti,Vanessa, Shilole, Beca, Baby J na wengine na amekuwa akimudu zaidi kuandika nyimbo zinazoimbwa na wasanii wa kike na kumfanya apendwe sana na wanawake.
Wakati mashabiki wa mziki wa Bongo Flava wakisubiria Tuzo za Kili Music Award, msanii AY amewataka waandaaji wa tuzo hizo kushirikiana na vyombo vya habari ili kuweza kupata siku nyimbo hizo zilipotoka ili kuepusha migongana kwenye kupanga vipengele, pia amezungumzia ishu ya video yake ambayo imeanza kuchezwa Jamaica baada ya bodi ya nchi hiyo kuipitisha.
Story ya mwisho kusikika ni ya star Ney Wa Mitego ambae wiki hii ameweka wazi majibu yake ya HIV, Ney amesema alikuwa hajaumwa muda mrefu lakini hivi karibuni aliumwa na kwenda Hospitali na kuamua kupima kila kitu kani yeye kama msanii na balozi wa vijana, anauwezo wa kuwashawishi vijana wenzake kwenda kupima na kwa sasa ameamua kutulia kwenye mstari mmoja na kuangalia familia yake.
No comments:
Post a Comment