Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiwaeleza
wahariri wa vyombo vya habari nchini wajibu na umuhimu wa vyombo vya habari katika mchakato huu wa
upatikani wa katiba mpya ikiwemo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa mchakato huu kwa
mustakabali wa Taifa pia alivipongeza vyombo vya habari katika elimishaji wa
wananchi katika mchakato wa Bunge Maalum la Katiba, Wakati wa Mkutano na
Wahariri wa Vyombo vya Habari Leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la wahariri Absalom Kibanda akiongea wakati wa mkutano
uliowakutanisha wahariri wa vyombo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamduni na
Michezo ambapo Dkt. Fenela Mukangara ambapo waliwataka wahariri kuwa wamoja
katika masuala ya kitaifa hasa yatakayopelekea kuibomoa nchi yetu pia aliwaasa
wahariri kutumia kalamu zao vizuri kuwaelimisha wananchi katika mchakato huu wa
kuelekea upatikaji wa Katiba Mpya kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya
Habari Bw. Assah Mwambene, Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mh.Angela
Kairuki na Mwisho ni Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara Leo Jijini Dar es Salaam.
Mzee
Kingunge Ngombale-Mwiru akiongea na wahariri wa vyombo vya habari ambapo ambapo
aliwaeleza kuhusu umuhimu wa upatikanaji wa katiba mpya kwa maendeleo ya Taifa
ikiwa katiba iliyopendekezwa imezingatia Masuala muhimu ya ukuzaji uchumi wan
chi pia uzingatiaji wa makundi mbalimbali katika jamii na alisisitiza umuhimu wa
vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kuelekea upatikanji wa katiba mpya kwani
katiba ni chombo cha ukombozi wa nchi.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la wahariri Absalom Kibanda akisalimiana na Mzee Kingunge
Ngombale-Mwiru wakati wa mkutano wa wahariri wa vyombo vya Habari na Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Mh.
Hamadi Rashid Muhamed akiwaeleza wahariri wa vyombo vya habari ambapo alieleza
furaha yake kwa katiba inayopendekezwa kujikita katika kutatua changamoto za
muungano zitakazopekea kuimarika kwa muungano wa Tanzania bara na Zanzibar.
Baadhi
wa Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini Wakifuatilia Mada zilizokuwa
zinawasilishwa katika mkutano huo
.jpg)





No comments:
Post a Comment