Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP, Thobias Sedoyeka, akitoa
taarifa ya wananchi kumuua kijana Hussein Jumanne Kisuke (31) anayedaiwa
kuwa ni jambazi sugu. Baada ya kumshambuliwa kwa silaha za jadi na
kufariki dunia na kisha kumchoma moto.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
Mtuhumiwa
wa Ujambazi mkazi wa Misuna Hussein Jumanne Kisuke (31) juzi alipigwa
na wananchi wa Misuna mjini Singida kwa kutumia silaha za jadi na
kuuwawa na kisha kuchomwa moto.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida, ACP, Thobias Sedoyeka, alisema tukio hilo
limetokea juzi saa 5.15 asubuhi huko katika maeneo ya Kipungua kata ya
Misuna tarafa ya Mungumaji manispaa ya Singida.
Alisema Kisuke alikuwa akitafutwa muda mrefu kuhusiana na tuhuma mbalimbali za ujambazi na wizi wa pikipiki.
“Kwa
ujumla Hussein Kisuke alikuwa mzoefu wa matukio ya unyang’anyi wa
kutumia silaha katika mji wa Singida. Siku ya tukio wananchi walimuona
akipita katika maeneo ya Kipungua na hivyo kumvamia na kuanza
kumshambulia kwa kutumia silaha za jadi na kisha kumchoma moto”alisema
Sedoyeka.
Kamanda
huyo alisema hadi sasa hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusiana na mauaji
hayo kwani wananchi waliojichukulia sheria mkononi,walitorokea
kusikojulikana baada ya kufanya mauaji hayo.
Sedoyeka
ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuacha mara moja tabia ya
kujichukulia sheria mkononi na badala yake watoe taarifa polisi,ili
mtuhumiwa/watuhumiwa wakamatwe na kufikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment