Kuna
taarifa zilitoka on millardayo.com leo jioni kuhusu msanii wa muziki wa
kizazi kipya Chidi Benz kukamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akiwa anaelekea Mbeya
kwenye show ya Instagram Party ambayo inatarajiwa kufanyika kesho.
millardayo.com iliahidi kuzifatilia hizi
taarifa kwa Polisi ili kupata uthibitisho ambapo imefahamika ni kweli
msanii huyu amekamatwa leo mchana akiwa katika sehemu ya kuondokea
uwanjani hapo ambapo baada ya alifanyiwa upekuzi na kubainika amebeba
dawa hizo ambapo ni kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati
lake na misokoto miwili ya bangi.
Amesema ‘Alikuja Airport kwa ajili ya
safari kwenda Mbeya, kete hizo 14 za dawa za kulevya zilikua
zimefungwafungwa na nailoni na pia amekutwa na vifaa vingine
vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za kulevya, kuna kigae na kijiko
na yeye mwenyewe anakiri ni vitu vyake huwa anatumia ila anashangaa ni
kwa nini vimeweza kubaki kwenye mfuko, tutamfikisha Mahakamani baada ya
kuweza kubaini ni dawa aina gani za kulevya’
Sauti ya Kamishna Hamis Sulemani akithibitisha tukio hilo unaweza kuisikiliza hapa.
No comments:
Post a Comment