Godfrey David Manent0 ambaye ni mtoto wa 4 wa marehemu David Manent0 kwenye exclusive interview na millardayo.com na kusema ‘Mzee wetu alikua akisumbuliwa na Lishe hali hii ilianza baada ya mama yetu kufariki miaka 2 iliyopita’
‘Si kwamba alikua hapati chakula vyakula vilikuwepo vya kutosha lakini alikua anakosa mtu wa kumpa matunzo ya ndani ya nyumba kama mke kwa hiyo tangu afariki mama mzee alikua mpweke’
‘Matatizo ya mzee mbali na kuwa na umri mkubwa pia alikua ni presha na alikua akisema mimi nina presha jamani baadae presha ikatengeneza kitu kama kisukari ikitokea presha inapanda na sukari inapanda baadae akawa anasema hadi miguu ina ganzi kidogo’
‘Mpaka mauti yanamfika tulishampeleka mara t3 hospitali na tulikua tukirudi,sisi kwenye familia tulikua 10 lakini 1 alifariki hivyo tumebaki 9,Mpaka sasa taratibu za mazishi tunaendelea kuzipanga’
‘Baba yetu sisi alikuwa mwenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro wilaya ya Same maeneo ya Mamba Miamba tulikuwa tunafikiria anaweza kuzikwa nyumbani kwenye asili yetu au tumzike hapa hapa Dar es salaam’
‘Siku za mwisho za Mzee wetu kama alikua akikiona kifo kwa sababu siku zake za mwisho mwisho alikua akisema jamani mimi naona kama sitopona alikua hana wasi wasi na kifo nadhani na ule uzee alikua akiuona na kuona siku zake zinakaribia’.
Mzee Manento amefariki akiwa na umri wa miaka 73 na kuacha watoto 9,filamu alizocheza enzi za uhai wake ni pamoja na Hero of the church,Dar To Lagos,Fake Pastor na zingine nyingine.
No comments:
Post a Comment