Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Jumanne Mbepo (kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi
milioni 15 ili kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 Mratibu wa mbio hizo
Bw. Mathew Kasonta (kushoto) katika hafla ya kukabidhi hundi hiyo na kutangaza
rasmi zawadi zitakazotolewa katika mbio hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Jana. Mbio hizo zitafanyika mkoani Mwanza, katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe
26 mwezi Oktoba mwaka huu. NSSF ikiwa kama mdamini mkuu wa mbio hizo.
Mratibu
wa mbio za Rock City Marathon 2014 kutoka Capital Plus International (CPI), Bw.
Mathew Kasonta (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 15 iliyotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 na kutangaza rasmi zawadi
zitakazotolewa katika mbio hizo jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo
zitafanyika mkoani Mwanza, katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 mwezi Oktoba
mwaka huu. NSSF ikiwa kama mdamini mkuu wa mbio hizo. Wakishuhudia katikati ni Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Bw. Jumanne Mbepo na Afisa Uhusiano wa NSSF, Bi. Anna Nguzo
(Kulia).
Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Jumanne Mbepo (Katikati) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni
15 kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 na kutangaza rasmi zawadi
zitakazotolewa katika mbio hizo jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo
zitafanyika mkoani Mwanza, katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 mwezi Oktoba
mwaka huu. NSSF ikiwa kama mdamini mkuu wa mbio hizo. Wakishuhudia kushoto ni
Mratibu wa mbio kutoka Capital Plus International (CPI), Bw. Mathew Kasonta na
Afisa Uhusiano wa NSSF, Bi.. Anna Nguzo (Kushoto).
NSSF
yanogesha mbio za Rock City 2014
Zawadi nono zatangatazwa kwa washindi
Zawadi
za washindi wa mbio za Rock City zitakazofanyika katika mkoa wa Mwanza tarehe
26 mwezi huu zimetangazwa jana huku mdhamini mkuu wa mbio hizo, Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) likitoa shilingi milioni 15 kuboresha mbio
hizo.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 15 kwa waratibu wa mbio
hizo, Capital Plus International Limited, Afisa uhusiano wa NSSF, Bw. Jumanne
Mbepo amesema kuwa NSSF imeendelea kudhamini mbio hizi kwa mwaka wa sita
mfululizo kutokana na kuona maboresho yanayofanyika katika mbio hizo kila
mwaka.
“Mbio
hizi zitaambatana na kutoa elimu kwa wakulima na wachimbaji wadogowadogo wa
madini katika kanda ya ziwa, juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko wa NSSF ili
waweze kunufaika na huduma zitolewazo na shirika kama vile mkopo, bima ya afya
pamoja na mafao mbalimbali,” Alisema Bw. Mbepo.
Mratibu
wa mbio hizo, Bw. Matthew Kasonta amesema kuwa udhamini huo utasaidia kwa kiasi
kikubwa kufanikisha maandalizi ya mbio hizo na kuleta maboresho makubwa katika
mbio za mwaka huu. Amesema kuwa maboresho hayo ni pamoja na kuwepo kwa mbio
fupi zitakazo jumuisha vijana kutoka katika shule za
sekondari na wale waliopo shule za msingi madarasa ya juu.
“Baada
ya kupata udhamini huu, tunafaraja ya kutaja zawadi watakazopatiwa washindi.
Kwa mbio za Kilomita 21, jumla ya shilingi milioni saba na laki moja zimetengwa
kwa ajili ya washindi. Washindi wa kwanza watazawadiwa Tsh 1.5m/- huku washindi
wa pili watapata laki tisa na washindi wa tatu watapata laki saba kila mmoja.
Kwa
mbio za kilomita tano, zaidi ya shilingi laki nne zimetengwa kwa ajili ya
washindi. Jumla ya shilingi laki tatu na arobaini zimetengwa kwa ajili ya
washindi wa mbio za kilomita 3 na shilingi laki mbili imetengwa kama zawadi kwa
ajili ya mbio za watoto za kilomita mbili.”
Bw.
Kasonta amesema kuwa kwa mbio fupi ambazo zimeanzishwa mwaka huu (mita 100,
mita 400 na mita 1,500) jumla ya shilingi laki nne na themanini pesa taslimu
zimetengwa kwa ajili ya washindi huku washindi wote wa kwanza (wa kike na
kiume) watapata king’amuzi cha Continental Decoders.
Bw. Kasonta aliwataja wadhamini waliofanyikisha mbio hizo kuwa ni
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), TSN Group kupitia kinywaji chake
cha Chilly Willy, pamoja na African Barrick Gold, IPTL, Air Tanzania, New
Mwanza Hotel, Nyanza Bottling, Sahara Media Group, Continental decoders, New
Africa Hotel, PPF, Tanapa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
“Nawasihi
watu waendelee kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za usajili katika ofisi za kampuni ya Capital Plus International
Limited (CPI) jengo la ATC ghorofa ya tatu jijini Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Augustino Mwanza, Ofisi zote za wilaya za Michezo na Utamaduni mkoani
Mwanza na Uwanja wa Nyamagana,” alisema Bw. Kasonta.
No comments:
Post a Comment