MAPAMBANO MENGINE YA MAREKANI DHIDI YA EBOLA.

Ebola Screening Starts At O'Hare Airport
Licha ya kwamba Marekani imekuwa nchi ambayo imeweka rekodi ya kutibu watu wenye maambukizi ya ugonjwa huku wachache wakiripotiwa kufariki, bado imetangaza mkakati madhubuti ambao umewekwa ili kuhakikisha wanadhibiti Ebola.


Marekani imetangaza rasmi utaratibu mpya ambao unaowalazimu abiria wanaosafiri kwa ndege kuingia nchini humo wakitokea Afrika Magharibi, kushuka katika moja ya viwanja maalum vitano ambavyo vimetengwa.
Utaratibu ambao Marekani imeuweka unawalazimu wasafiri wote kutoka nchi za Liberia, Guinea na Sierra Leone kuingia nchini humo kwa kupitia moja viwanja vya O’Hare Chicago, JFK, Newark, Washington Dulles au Atlanta.
         Chicago_O'Hare
Marekani imeweka utaratibu huo ambapo viwanja hivyo vina wataalamu na mashine maalum za kufanyia uchunguzi wa virusi vya ugonjwa huo.
Leo kamati ya dharura ya shirika la afya duniani WHO imefanya mkutano huku lengo kuu likiwa ni kutathmini juhudi zilizofikiwa za kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Japo WHO imetangaza kutekeleza mpango wa chanjo ya kinga ya Ebola katika ukanda wa Afrika Magharibi matumaini bado ni madogo mpaka sasa ambapo zaidi ya watu 4,700 wameripotiwa kufariki kwa ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment