Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kutoka kulia) akitoa ufafanuzi wa kisheria mbele ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira. Kamati hiyo iko katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Sheria ya Mazingira katika Migodi. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mh. James Lembeli (wa tatu kulia), Mh. John Mnyika na Mh. Henry Shekifu wajumbe wa Kamati hiyo. Wa kwanza (kushoto) ni Bw. Peter Burger, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu.
Pichani ni taka za plastiki zilizohifadhiwa vizuri kwa ajili ya urejelezwaji katika Mgodi wa Bulyanhulu.
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu wakati wa ukaguzi katika Mgodi huo kuona utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu mara baada ya ukaguzi katika Mgodi huo kuona utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.




No comments:
Post a Comment