TAZAMA PICHA 8 ZA WAFUASI WA CHADEMA NA CCM WALIPOCHAPANA MAKONDE JIJINI DAR MBELE YA WAZIRI WA MAJI NA JOHN MNYIKA
Mbunge
wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (KULIA), akiamulia ugomvi wa
Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa Chadema (kushoto) na Mwenyekiti wa
CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge waliotaka kuzichapa ulipotokea
mzozo katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla
katika Uwanja wa Shule ya Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo,
Dar es Salaam jana.
Wafuasi
wa CCM na Chadema wakitaka kuzipiga kavu kavu baada ya kutokea mzozo
ambapo wanaCCM walikuwa wakimzomea Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John
Mnyika akihutubia na WanaChadema wakimzomea Naibu Waziri wa Maji, Amos
Makalla akihutubia katika mkutano huo.
Poilisi
wakiwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipinga Mbunge wao John
Mnyika asijibu swali lililoulizwa na Mkazi wa Kibamba, Jordan Balindo
aliyemtaka Mnyika aeleze ni jitihada hani amezifanya binafsi kama mbunge
kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika jimbo la Ubungo.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo,
John Mnyika (Chadema), wakitofautiana jukwaani wakati Makalla akiamuru
polisi kuwatoa wafuasi wa Chadema waliokuwa wakimzomea wakati akileleza
Utakelezaji wa Ilani ya CCM JUU YA MAJI, HUKU mNYIKA AKITAKA WAENDEE
KUZOMEA AKIDAI KWAMBA WAZIRI HAKUFANYA HAKI KWANI YEYE ALIPOKUWA
AKIZOMEWA NA WANA CCM HAKUWACHUKULIA HATUA KAMA HIYO KATIKA MKUTANO WA
HADHARA ULIOFANYIKA KATIKA UWANJA WA SHULE YA MAVURUNZA, KATA YA SALANGA
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka, Dar es Salaam, EvaSinare
(katikati) akijaribu kuunusuru mzozo huo kwa kuzungumza na Naibu Waziri
wa Maji, Amos Makalla 9kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John
Mnyika.
Polisi akilinda usalama mbele ya mashabiki wa CCM na Chadema
Wafuasi wanawake wa CCM na Chadema wakichimbia mkwara.
Mfuasi wa Chadema akiwa na bango la kuishutumu Serikali
Mfuasi wa CCM akiwa na bango la kumshutumu Mbunge wa Jimbo hilo, John Mnyika.
No comments:
Post a Comment