TATIZO LA MAJI KATIKA MJI WA SENGEREMA IMEKUWA CHANGAMOTO INAYOWAKABILI WANANCHI KATIKA MJI WA SENGEREMA.
MAJI YAMEKUWA YAKITOKA KWA MGAO KILA MTAA MGAO ULIKUWA NI MALA TATU KWA WIKI KWA KILA MTAA LAKINI KWA SASA IMESHINDIKANA IMEKUWA NI MALA MOJA KWA WIKI LAKINI PIA KUNA MAENEO MENGINE WAMEKUWA HAWAPATI KABISA HATA KWA HUO MGAO WA MALA MOJA KWA WIKI.
WAKATI MWINGI HATA YAKITOTA YANATOKA USIKU SANA HALI INAYOWAFANYA WANANCHI WENGI KUWA NA WASIWASI NA USALAMA WAO KWANI WASIOKUWA NA MABOMBA KATIKA NYUMBA ZAO WANALAZIMIKA KUYAFATA MBALI KIDOGO, WAKATI MWINGINE YANAPOKUWA YAMETOKA YANASABABISHA WANANCHI KUPIGANA VIKUMBO NA HATA NGUMI ILI KUCHOTA MAJI.
LAKINI PIA HATA YANAPOTOKA YAMEKUWA HAYAKAI KWA KIPINDI KIREFU HALI INAYOSABABISHA KUWE NA MSURURU MKUBWA WA FOLENI YA MADUMU WAKATI MWINGINE WATU WAMEKUWA WAKIACHA VITU ILI KULINDA FOLENI ZAO ILI PINDI YATAKAPOTOKA IWE RAHISI KUCHOTA.
HAPA NI SEHEMU MOJA TU YA ENEO TULILOPIGA PICHA LINALOPATIKANA IBISABAGENI BARABARA YA BUSISI ROAD KARIBU NA SHELI YA MOSHA.
HII NDIO HALI HALISI ILIVYO KATIKA MAENEO MENGI YA KUUZIA MAJI.
HUYU MAMA AKIWEKA MAJI KATIKA VYOMBO VYAKE AKIWA NA MTOTO WAKE ALIEKUJA KUSAIDIANA NAE KUTEKA MAJI.
MAJI YAKITOKA KWA KASI NDOGO SANA AMBAYO HAIWEZI KUKIZI MAHITAJI YA WANANCHI HAWA.
VYOMBO VIKIWA KATIKA FOLENI YA MAJI NA FOLENI NI KUBWA LAKINI MAJI YANATOKA KWA KASI KIDOGO SANA.
MAJI YANAELEKEA KUKATIKA LAKINI FOLENI BADO NI KUBWA SANA.
RAI YETU KWA UONGOZI NA MAMLAKA HUSIKI KUJITAHIDI KWANZA KUTOA MAJI MAPEMA LAKINI PIA KUJITAHIDI KUPUNGUZA MGAO WA MAJI ILI UENDANE NA MAHITAJI YA WATU.LAKINI PIA TUNASHUKURU HATA KWA HAYA MAJI YANAYOTOKA KWANI HALI INAWEZA KUWA MBAYA SANA.
No comments:
Post a Comment