Habari za ndani
zilieleza kuwa polisi wa Kituo cha Tabata-Shule, Dar ndiyo wamemtaka
kujisalimisha baada ya binti anayedaiwa kubakwa kufungua jalada kituoni
hapo lenye namba TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada la Uchunguzi namba
TBT/IR/1865/2014 akidai kutendewa unyama huo kwa siku mbili (Ijumaa na
Jumapili wiki mbili zilizopita).
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho ndani ya jeshi hilo, zoezi la
kumsaka limeanza tangu Mei 19, mwaka huu aliposhitakiwa na shemejiye
kituoni hapo lakini hadi gazeti hili linakwenda mitamboni Jumamosi
jioni, jitihada zilikuwa hazijazaa matunda.
Ilisemekana kwamba licha ya kuweka mikakati kabambe ya kumtia nguvuni
ili ahojiwe kuhusiana na tuhuma hizo huku jeshi hilo likimtaka Mbasha
kujitokeza kabla nguvu nyingi hazijatumika.
“Tunamtaka ajitokeze mwenyewe kabla hatujatumia nguvu nyingi kumsaka,
maana jeshi lina mkono mrefu hivyo hana ujanja na ukizingatia yeye ni
mtu maarufu,” kilisema chanzo.
Ilidaiwa kuwa, Mbasha alitoweka nyumbani kwake, Tabata-Kimanga wakati
ambao mkewe (Flora) alikuwa amehamia hotelini kutokana na ugomvi mzito
waliokuwanao.
Taarifa zaidi zilisema, kwa kuwa mlalamikaji alifikisha malalamiko
hayo polisi akiwa na viambatanisho vya vipimo vya daktari vilivyoonesha
kuingiliwa kimwili kwa nguvu, Mbasha anatakiwa ajitokeze ili kutoa
maelezo ya upande wake na taratibu za kisheria ziendelee.
Jitihada za kumpata Mbasha zilishindikana kwa kuwa simu yake haipo hewani kwa siku kadhaa sasa.
No comments:
Post a Comment