WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAMEVAMIA DUKA LA UREMBO HAPA SENGEREMA LILILOPO BARABARA YA PAMBALU KARIBU NA MZAMBARAU.
MAJAMBAZI HAO WALIFIKA KATIKA ENEO HILO MUDA WA SAA MBILI KASORO NA KUVAMIA DUKA LA BWANA FRANKE MADUKA . BAADA YA KUFIKA PALE NA KUMLAZIMISHA KUTOA PESA NDIPO ALIPOANZA KUPIGA KELELE ZA KUVAMIWA HALI ILIYOPELEKEA MAJAMBAZI HAO KUMPIGA RISASI YA MKONONI.
BWANA FRANKE ALIFANIKIWA KUKIMBIA LAKINI KWA BAHATI MBAYA ALIPIGWA TENA RISASI YA KIFUANI UPANDE WA KUSHOTO ILIYOPELEKEA KUTOKA DAMU NYINGI ZILIZOPELEKEA KUKOSA NGUVU NA KUDONDOKA CHINI.
KWANI KWA MUDA WA TUKIO WATU BADO WALIKUWEPO KATIKA ENEO HILI HIVYO WAKAWA WAMEMCHUKUA NA KUMPELEKA KATIKA HOSPITAL YA MISSION ILIYOPO HAPA SENGEREMA. BAADA YA KUFIKA HOSPITAL ALICHUKULIWA PICHA YA X-RAY NA MADAKTALI KULAZIMIKA KUMHAMISHIA KATIKA HOSPITAL YA BUGANDO MWANZA KWA MATIBABU ZAIDI .
LAKINI PIA KATIKA DUKA HILO LA UREMBO BWANA FRANKE ALIKUWA NA MKEWE ALIEPOTEZA FAHAMU BAADA YA TUKIO LA MUMEWE KUPIGWA RISASI KWANI INASEMEKANA ALIKUWA AKIYASIHI MAJAMBAZI HAYO YASIMUUE MUME WAKE.
ENEO HILO LIMEZUNGUKWA NA WALINZI WENGI WA KAMPUNI MOJA LA ULIZI JINA TUNALO LAKINI CHA KUSHANGAZA PAMOJA NA WALINZI HAO KUYAONA HAYO MAJAMBAZI MAWILI NA JAMBAZI MOJA NDIO LILILOKUWA NA SILAHA LAKINI WALINZI HAO KWA WINGI WAO WALIKIMBIA NA KUACHA MAENEO YAO YA ULINZI YAKIWA WAZI NA CHA KUSHANGAZA NI KWAMBA WALINZI HAO HUWA NA SILAHA LAKINI KATIKA TUKIO HILO HAKUKUWA NA MLINZI ALIEKUWA NA SILAHA ISIPOKUWA WALIKUWA NA MARUNGU.
BAADA YA MDA WALIKUJA ASKALI WA JESHI LA POLISI NA KUHAKIKISHA WANAWEKA ULINZI WA KUTOSHA KATIKA ENEO LA TUKIO NA NA KUHAKIKISHA DUKA LINAFUNGWA NA TARATIBU ZA KIUSALAMA ZIKIENDELEA.
MAJAMBAZI HAYO BAADA YA KUMALIZA KAZI YAO YALIONDOKA TENA KWA KUTEMBE KWA MIGUU NA HAIFAMIKA WALIKUWA NA USAFIRI GANI, LAKINI KWA HABARI TULIZOPATA KWA MASHUHUDA WA TUKIO WALITUELEZA KUWA MAJAMBAZI HAO WAWILI BAADA YA KUTOKA HAPO DUKANI WALIKWENDA KUPANDA PIKIPIKI AMBAYO HATUFAHAMU KAMA WALIKODI AU VIPI
HIVYO TUNATOA POLE KWA FAMILIA YA BWANA NA BIBI FRANKE KWA TUKIO LILILOWAPATA NA MUNGU AMSAIDIE BWANA FRANKE APONE NA KURUDIA HALI YAKE YA KAWAIDA MAOMBI YENU YATASAIDIA KATIKA KUHAKIKISHA BWANA FRANKE AKIRUDI KATIKA HALI YAKE YA AWALI.
TUNAPENDA KUWAOMBA WANANCHI WA SENGEREMA KUWA NA UTULIVU WAKATI JESHI LA POLISI LIKIENDELEA NA UCHUNGUZI WAO KWANI TUNAIMANI NA JESHI LETU NA LITAFANIKIWA KATIKA KAZI YAKE NA PIA WANANCHI NI VIZURI MKASHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KUHAKIKISHA WATU HAO WANAPATIKANA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.
TUNAPENDA KKUTOA RAI YETU KWENU UNAPOCHANGIA MJADALA HUU JITAHIDI KUJIEPUSHA NA MANENO YASIJENGA ZAIDI YA KUBOMOA KIKUBWA NI KUTOA MAONA AMBAYO HAYATAMUMIZA MTU YOYOTEA KATIKA FAMILIA NA WATU WENGINE.
TUTAKUWA TUKIWALETEA MUENDELEZO WA HABARI HII KADRI TUTAKAVYOKUWA TUNAIPATA.
ENDELEA KUTEMBELEA BLOG YETU KWA HABARI MBALIMBALI.
Dah! nawapa pole familia ta Frank, Mungu na awape afya njema
ReplyDelete