Huku idadi ya nchi zinazopinga watu kujihusisha na ngono za jinsia moja ikizidi kuongezeka, serikali ya Marekani imeanzisha kampeni ya kutetewa na kuungwa mkono kile inachokiita 'haki' za watu wanaolawitiana na kusagana. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani John Kerry ametoa radiamali kali kuhusu sheria iliyopitishwa hivi karibuni na serikali ya Uganda dhidi ya watu wanaolawitiana na kusagana na kudai kwamba sheria hiyo inafanana na sheria za kipindi cha utawala wa Wanazi nchini Ujerumani dhidi ya Mayahudi na pia sheria za ubaguzi wa rangi dhidi ya weusi Afrika Kusini. Kerry amesema anakusudia kutoa agizo kwa mabalozi wa Marekani katika nchi tofauti kuanza kuchunguza changamoto hiyo katika uga wa kimataifa.
Serikali ya Marekani imeanza kukabiliana na sheria dhidi ya vitendo vya liwati na usagaji kupitia vyombo vyake vya kidiplomasia, wakati nchi nyingi duniani zimeonyesha kuvipinga na kuchukizwa na vitendo hivyo vichafu. Dini zote za mbinguni, kuanzia dini ya Kiyahudi, Kikristo na Kiislamu, zinavitaja vitendo vya liwati na usagaji kuwa vinakinzana na misingi ya kidini, ubinadamu na maadili. Hapana shaka kuwa mabilioni ya watu duniani wanapinga vikali vitendo hivyo vya liwati na usagaji. Kwa uchache, nchi 80 duniani ambazo ni zaidi ya theluthi moja ya nchi zote duniani, zimeweka sheria ya kupiga marufuku vitendo hivyo vya kihayawani. Hata baadhi ya nchi ambazo zinafuata misingi ya demokrasia ya uliberali, zinakerwa na vitendo hivyo, na wananchi walio wengi kwenye nchi hizo wanaamini kwamba mahusiano ya ngono ya watu wenye jinsia moja hayapasi kutambuliwa kuwa ni ndoa. Jamii hiyo ya walimwengu inaamini kwamba, ndoa inatambuliwa rasmi kwa watu wa jinsia mbili tofauti.
Suala hili la eti ndoa ya watu wa jinsia moja, limetoa changamoto kubwa ya kijamii na kisheria katika ulimwengu wa Magharibi. Pamoja na hayo, baadhi ya nchi za Magharibi zinafanya njama, ili mataifa mengine duniani yafuate kibubusa mtindo wa maisha wa Kimagharibi. Hivi sasa inaonekana kuwa nchi za Asia na Afrika zinalazimishwa kufuata maisha ya Wamagharibi, kinyume cha hivyo zitakabiliwa na tuhuma kama vile ukiukaji wa demokrasia na haki za binadamu. Katika nusu ya karne iliyopita tumeshuhudia mashambulio ya kijeshi na anuwai za mapinduzi yaliyofanywa na nchi za Magharibi katika nchi za ulimwengu wa tatu, kwa kisingizio cha kutetea demokrasia na haki za binadamu. Inaonekana kuwa katika miongo hii ya mwanzoni mwa karne ya ishirini na moja, nchi za Magharibi zimeibuka na ajenda mpya ambayo inafanywa kuwa kisingizio cha kukana na kufuta itikadi, mtindo wa maisha, sheria na kanuni, pamoja na mila na desturi za nchi nyengine.
Kwa minajili hiyo, kwenye ulimwengu huu usio na amani na uliogubikwa na vita, umasikini, ukandamizaji, dhulma na mabalaa ya njaa, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani anathubutu kulitaja suala la kupitishwa sheria dhidi ya liwati na usagaji nchini Uganda, kuwa ni sawa na vitendo vya kuuliwa Mayahudi wa Ulaya na ubaguzi wa rangi dhidi ya weusi Afrika Kusini. Kerry amefikia hatua ya kutishia kwamba, kuna ulazima wa kuchukua hatua kali za kidiplomasia za kukabiliana na sheria zilizo dhidi ya liwati na usagaji. Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa, huenda tukaanza kushuhudia katika siku za usoni mashambulio ya kijeshi ya Marekani na Ulaya dhidi ya nchi za Asia na Afrika kwa kisingizio cha kutetea kile kinachoelezwa kuwa ni haki za wanaolawitiana na wanaosagana.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, miaka 150 iliyopita, Wazungu, ambao hivi sasa wanajinadi kuwa ni vinara wa kupambana na dawa za kulevya, waliushambulia ufalme wa China, ili uruhusu utumiwaji wa afyuni nchini humo. Vita hivyo vilijulikana katika historia kama 'vita vya afyuni'. Kwa minajili hiyo, ni jambo lisilo mbali kuziona nchi za Magharibi vikianzisha 'vita vya kutetea 'liwati na usagaji' duniani na kumwaga damu nyingi za watu wasio na hatia.

No comments:
Post a Comment