Mazishi ya mganga wa kienyeji mwanasana katika wilaya ya sengerema.

   Hapa watu mbalimbali waliojitokeza kushuhudia aina ya mazishi ya waganga inavyokuwa kwani wengi hawajawahi kuona.
  Makabuli ya waganga wa kienyeji huwa yanakuwa ya mduara na hili ndio kabuli alilozikwa mwanasana  na kwa ndani unavyoona tayari kazikwa kwa kukalishwa katika kigoda akiwa kakalishwa na huo ni udongo uliowekwa ndani pamoja na kamba zinazoonekana nyeupe.
 Hapa wajukuu wakiweka mashada katika kabuli la marehemu bibi yao mpendwa mwanasana wakionekana wakiwa wamejifunga vitambaa vyeupe kwa mila za kiganga.
  Hapa pia wajukuu wakiwa wamejifunga vitambaa vyeusi wakiweka mashada
 Hapa wakimalizia zoezi la kuweka mashada. Lakini samahani hatutaweka video inayoonyesha zoezi zima lilivyokuwa kwa sababu zilizo nje na uwezo wetu na kwa mashariti ya taaluma ya waganga pia hatukuweza kuweka picha za mwili jinsi ulivyo kuwa ukiwekwa na kukalishwa katika kigoda ndani ya kabuli. Marehemu kafikwa na umauti akisumbuliwa na ugonjwa wa presha tarehe 25/10/2013 katika hospitali ya DDH sengerema mission. Mungu aipumzishe roho ya marehemu bibi yetu ameen.

No comments:

Post a Comment