Siku moja tu baada
ya Umoja wa Afrika kutangaza kwamba utawapeleka waangalizi 100 wa haki
za kibinaadamu pamoja na waangalizi wengine 100 wa kijeshi nchini
Burundi,
Sasa umoja wa mataifa pia unasema kuwa utawapeleka
maafisa wake wa upelelezi nchini humo ilikutathmini iwapo kuna visa
vyovyote vya ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo.Taarifa ya Umoja wa mataifa inasema kuwa wachunguzi 3 kutoka Algeria, Colombia na Afrika Kusini watafanya shughuli yao kwa juma moja kuanzia Machi tarehe mosi.
UN inasema kupitia kwa taarifa yake kuwa inalenga kuchunguza na kubaini wale wanaochochea na kupanga matukio ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu nchini humo.
Afisa wa umoja huo bwana Christof Heyns anasema ripoti ya watatu hao itakuwa huru.
Burundi imekumbwa na machafuko tangu Nkurunziza atangaze nia ya kuwania muhula wa tatu Aprili mwaka jana.
Wapinzani wake wanadai kuwa muhula huo wa tatu unakiuka katiba ya nchi.
Lakini Nkurunziza anadai kuwa muhula wa kwanza aliotawala ilikuwa ni kipindi cha mpito kufuatia mazungumzo ya amani.
chanzo bbc.


No comments:
Post a Comment